Na Kalonga kasati
Umoja wa vijana wa chama chama cha mapinduzi mkoa wa
kigoma(UVCCM)wamefanya usafi katika hospitali ya mkoa maweni sambamba na
kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika wodi mbalimbali hospitalini hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi
msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
mbunge wa viti maalum kupitia umoja huo wa vijana Zainabu Katimba
alisema kuwa wameamua kuwafariji wagonjwa na kufanya usafi hospitalini hapo ili
kuendana na kasi yam he Rais john pombe magufuli wa hapa kazi tu.
Sisi kama vijana tumeamua kusherekea kauli mbiu ya mhe
Rais magufuli ya hapa kazi tu kwa
vitendo hii si kwa ajili ya siku ya uhuru tu kesho hili ni zoezi endelevu
tutakuwa tunalifanya mara kwa mara alisema Bi Katimba.
Aliwataka wananchi wote bila kujali itikadi zao
kumuunga mkono Mhe Rais kwa kujitokeza siku ya kesho na kufanya usafi katika
maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuepekana na maradhi ya milipuko
kama kipindupindu na mengine.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa vijana (uvccm) mkoa Peter
Msanjile alisema kuwa na zoezi hilo la usafi katika maeneo mbalimbali
linatekelezwa na vijana katika mikoa
yote
Msanjile amempongeza Rais wa awamu ya tano John pombe
magufuli kwa kazi nzuri anazofanya kwa kuwajibisha wahujumu uchumi
No comments:
Post a Comment