Tuesday, December 22, 2015
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Balozi wa Rwanda Hapa nchini Eugene Kayihura aliyefika Ikulu kwa
ajili ya mazungumzo.
RAIS
Paul Kagame wa Rwanda amefurahishwa na Hatua ambazo Rais John Magufuli Anazichukua, Hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa bandari huku
akimhakikishia kuwa Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania, hasa
katika kuitumia Bandari ya Dar es Salaam.
Siku
chache baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli akimtumia Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa, alifanya ziara ya ghafla katika Bandari ya Dar es
Salaam, ambako alifichua ufisadi wa mabilioni ya shilingi kutokana na
upotevu wa makontena, ambayuo hayakulipiwa kodi stahili kwa serikali.
Kutokana
na ufisadi huo, Rais aliivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari (TPA), alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA,
Awadhi Massawe na kusimamisha Maofisa kadhaa wa bandari Hiyo na wengine
wanaohusika na usimamizi wa Bandari kavu.
Aidha, Alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Rished Bade na maofisa wengine wa mamlaka hiyo, ambao miongoni mwao
tayari wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Dar es Salaam kutokana na ubadhirifu huo.
Kutokana
na hilo, Rais Kagame kupitia kwa Balozi wake nchini, Uegene Kayihura, Amempongeza Rais Magufuli kwa Hatua Alizochukua kusafisha Uozo katika Bandari Hiyo, ambayo Rwanda inapitisha asilimia 70 ya mizigo yake. Dk
Magufuli Jana alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi Kayihura Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Katika
mazungumzo hayo, Balozi Kayihura aliwasilisha salamu za pongezi kutoka
kwa Rais Kagame ambaye alimpongeza Dk Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais
wa Awamu ya Tano wa Tanzania.
Kwa
mujibu wa Balozi Kayihura, Rais Kagame Amefurahishwa na Hatua ambazo
Rais Magufuli anazichukua Hasa katika Usimamizi na utendaji kazi wa Bandari na kumhakikishia kuwa Rwanda iko Tayari kushirikiana na Tanzania
hasa kuitumia Bandari ya Dar es salaam ambayo hupitisha Asilimia zaidi
ya 70 ya mizigo ya Rwanda.
Aliongeza
kuwa Rwanda na Tanzania ni nchi Marafiki na Majirani, hivyo kuna kila Sababu ya kujenga Ushirikiano Madhubuti katika Sekta ya Uchumi.
Rais
Magufuli Alimuomba Balozi Kayihura, kumfikishia Rais Kagame Salamu za
shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania na kwamba Amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda.
Alimhakikishia
Balozi Kayihura kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano, itaendelea
kushirikiana na Rwanda ili Wananchi wa nchi Zote Mbili Wanufaike
kimaendeleo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AFDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika
hatua Nyingine, Dk Magufuli Amemhakikishia Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika, Dk Tonia Kandiero kuwa Serikali yake itaendelea
kushirikiana na Benki Hiyo katika Utekelezaji wa ,Miradi Mbalimbali ya Maendeleo.
Dk Magufuli alisema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya Mazungumzo na Mwakilishi huyo.
Pamoja
na kumhakikishia Ushirikiano, Rais Magufuli alitoa Mwito kwa Benki hiyo
kupunguza Michakato ya kuelekea katika Utekelezaji wa miradi na Badala
yake Ameshauri Uwepo Utaratibu wa Haraka Unaowezesha kuanza kwa miradi
katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa.
Kwa
upande wake, Dk Kandiero pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa
kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Awamu ya Tano, Amemhakikishia kuwa benki iko tayari kuendelea
kushirikiana na Tanzania katika Maendeleo kama ambavyo imekuwa ikifanya
na kwamba kwa sasa imetenga Dola Bilioni 2.3 kwa ajili ya kufadhili Miradi Mbalimbali ya Maendeleo.
Alisema
katika mipango yake, ADB imelenga kujielekeza katika Utoaji wa Mikopo
katika Sekta ya nishati na Usafiri. Naye Dk Magufuli Aliipongeza ADB kwa
kuamua kujielekeza katika sekta hizo za Nishati na Usafiri na pia Aliisisitiza kuangalia Namna itakavyounga Mkono mradi wa Ujenzi wa Reli
ya Kati kwa kiwango cha kisasa.
No comments:
Post a Comment