Kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr, licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa
anaweza kutimuliwa Ndani ya kikosi hicho na nafasi yake kupewa kocha Wa
zamani wa Timu hiyo, Mserbia, Goran Kopunovic, ameibuka na kusema suala
hilo wala Halimtishi hata kidogo.
Hivi karibuni kuliibuka Taarifa za ndani ya Simba zikisema Uongozi Umempa Muingereza huyo Michezo ya Mzunguko wa kwanza iliyobakia
kuhakikisha anapata matokeo mazuri la sivyo Anaweza kuondolewa
kukioongoza kikosi hicho.
Akizungumza na Fofam media , Kerr Amesema Anachojiamini ni kwamba
kazi yake Anaifanya ipasavyo hivyo hata akitimuliwa ni kama Wanamuonea
tu.
“Hilo suala la kuondolewa wala Halinitishi Hata kidogo, nimekuwa
nikiifanya kazi yangu kwa Ufanisi lakini mazingira yanatunyima
kufanikiwa Na kupata ushindi.
“Kabla ya mechi yetu na Mwadui Tulikua tukifanya Mazoezi kwenye uwanja
mbovu ambao ni kama Sehemu ya malisho ya ng’ombe, kocha unatakiwa
kuiandaa timu katika hali nzuri ili mpate matokeo Mazuri. Pia siku moja
kabla ya mechi tulikwenda Uwanjani tukaukuta haupo katika kiwango
kizuri.
“Binafsi Hata Mimi Matokeo haya yananiumiza, Mashabiki wengi kutoka Dar
walikuja kutusapoti lakini wameondoka Vichwa chini, Baada ya Mchezo.
Nilimuona Mwanadada akilia kwa Uchungu kisa Hatujapata Ushindi, hiyo
inaonyesha ni Jinsi gani mashabiki Wanaumizwa na Matokeo Mabaya,”
alisema Kerr.
Sare iliyoipata Simba, Juzi Jumamosi ni ya Tatu Mfululizo, ilianza
kutoka sare ya 2-2 Dhidi ya Azam kisha ikaambulia 1-1 na Toto Africans.
No comments:
Post a Comment