Uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji la Tanga Umezua Vurugu kubwa leo Baada ya Mkurugenzi wa Jiji hilo kumtangaza Mgombea wa CCM kuwa Mshindi licha ya Chama hicho kuzidiwa Idadi na Madiwani wa Chama cha Wananchi (CUF).
Madiwani
wa Ukawa wako 20 huku Madiwani wa CCM wakiwa 17, hivyo upande wa UKAWA
walikuwa na imani kuwa kwa wingi wao wangeweza kuongoza Halmashauri hiyo
kwa kupata kura nyingi.
Taarifa
za kuaminika kutoka katika chumba cha kupigia kura Zimeeleza kuwa Baada
ya Zoezi la kupiga kura, Mkurugenzi na Timu yake walihesabu kura zote
zilizopigwa na Baadaye alitangaza kuwa mgombea wa CCM ameshinda kwa
kupata kura 19 Dhidi ya Mgombea wa CUF Ambaye amepata kura 18.
Baada
ya tangazo hilo, vurugu kubwa Ilizuka ukumbini hapo Huku CUF wakidai
kuwa ilikuwa mbinu ya CCM kumtumia Mkurugenzi Wa Jiji hilo kuhujumu Uchaguzi na kumpa Ushindi Mgombea wake.
Zoezi
la kumchagua Meya wa Jiji hilo lilitanguliwa na Uchaguzi wa Naibu Meya
ambapo Mgombea wa CUF alitangazwa kuwa Mshindi kwa kupata kura 21 Dhidi
ya Mgombea wa CCM aliyepata kura 16, Matokeo Ambayo CUF wanadaiwa
kuyapinga Wakidai Yaliandaa mazingira ya Hujuma ya Meya.
“CUF Wanadai kuwa Mkurugenzi aliandaa Mazingira ili Ionekane kuwa kuna Diwani Mmoja wa CCM alimpigia kura mgombea wa CUF kwenye unaibu Meya,
ili baadae Aoneshe kuwa kuna wagombea wa CUF Waliompigia kura Mgombea wa
CCM na kumuwezesha kushinda,” Chanzo kimeiambia Fofammedia.
No comments:
Post a Comment