Saturday, 19 December 2015

Jeshi la Polisi latoa Onyo kali kwa Wanaosambaza Habari za Uongo katika Mitandao ya Kijamii Kupotosha Umma

Posterd Kalonga Kasati

Polisi_1_-_Msemaji_Msaidizi_wa_Jeshi_la_Polisi_Nchini_ASP_Advera_Senso_akitoa_ufafanuzi_kwa_waandishi_wa_habari_hawapo_pichani-e1427469063120Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera John Bulimba – SSP.

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Kwa Vyombo Vya Habari

Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka Tabia ya Baadhi ya watu kutoa Taarifa za Uzushi na Uongo kutumia Majina ya Taasisi, Mashirika ya Umma na ofisi za Serikali na kueneza Taarifa Hizo katika Mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha Wananchi.


Miongoni Mwa Taarifa Hizo ni pamoja na Taarifa Kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika Mitandao ya kijamii yenye kichwa cha Habari ‘Chujio Jeshi la polisi, vyeti Feki vyawaondoa Askari kazini’ Taarifa Hiyo ni Uzushi na Haijatolewa na Jeshi la Polisi.

Kufutia hali hiyo, Jeshi la Polisi Nchini linapenda kukanusha Taarifa Hiyo ya Uzushi ambayo haina Ukweli Wowote na Inalengo la kuchafua Taswira ya Jeshi la Polisi kwa Jamii.

Jeshi la Polisi Nchini limeanza Upelelezi wa kuwatafuta Watu Wote Waliohusika kueneza Taarifa Hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi. Aidha, Tunatoa onyo kali kwa Watu wote kuacha kutumia Mitandao ya kijamii Vibaya kwa kufanya Uposhaji Na Badala yake Watumia Mitandao Hiyo kwa Ajili ya Ustawi wa Jamii.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi. Makao Makuu ya Polisi.

No comments:

Post a Comment