Na Kalonga Kasati
Azam
Fc inamenyana na Majimaji Uwanja Wa Majimaji mjini Songea leo katika Mchezo Ambao ikishinda inarejea kileleni Mwa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.
Azam
FC ilishushwa kileleni na mabingwa Watetezi, Yanga SC baada ya ushindi
wa 1-0 Dhidi ya African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumatano.
Lakini
leo Azam FC inakutana na Majimaji Ambayo mchezo wa mwisho ilifungwa 5-1
na Vibonde wenzao Toto Africans Uwanja wa Majimaji.
Azam
FC inapewa nafasi kubwa ya kushinda Mchezo wa leo na kurejea kileleni
mwa Ligi Kuu, kutokana na ukweli kwamba Majimaji ni Timu Dhaifu.
Mabingwa
watetezi, Yanga SC nao pia Watashuka Dimbani Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam leo kumenyana na Stand United ya Shinyanga, ambayo hakika na timu
ngumu.
Ikitoka
kufungwa 2-0 nyumbani na Mwadui katika Mchezo wake uliopita, Stand
inayoongozwa na kinara wa mabao wa Ligi Kuu, Elias Maguri inatarajiwa
kupambana leo kuzinduka.
Nao mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC watakuwa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza leo kumenyana na Toto Africans.
Toto imekuwa na kawaida ya kuifunga Simba SC Uwanja wa Kirumba na hilo linafanya Mchezo wa leo, uvute hisia za wengi.
Simba
SC leo wanatarajiwa kuwa kamili, Baada ya wachezaji wake iliyowaingiza Dirisha dogo, Mganda Brian Majwega, Mkenya Paul Kiongera na wazalendo
Novat Makunga na Hajji Ugando kuruhusiwa kucheza.
Mechi
nyingine za Ligi Kuu leo ni kati ya Mwadui FC na Ndanda FC Uwanja wa
Mwadui Complex, Shinyanga, Kagera Sugar na African Sports Uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora na Prisons na Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya – wakati kesho JKT Ruvu Wataikaribisha Coastal Union Uwanja
wa Karume, Ilala, Dar es Salaam na Mbeya City Watakuwa wenyeji wa Mgambo
JKT Uwanja wa Sokoine.
No comments:
Post a Comment