Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo amesema kwamba Hawezi kuwavulilia Viongozi na Watendaji ambao Wanafanya Hujuma katika Mfumo wa Stakabadhi Ghalani
katika zao la korosho kwa Maslahi yao Binafsi Na Badala yake Suala
hilo atalivalia Njuga kwa kuwawajibisha kuwachukulia Hatua kali Za Kisheria ili iwe Fundishisho kwa Wengine Wenye Vitendo kama hivyo.
Kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa
ameitoa wakati wa mkutano Maalumu na Wadau wa zao la korosho wa Mkoa
wa Pwani wa kujadili Mwenendo mzima wa Mfumo wa kukunua zao Hilo kwa
kutumia njia ya Stakabadhi Gharani pamoja na changamoto Zinazowakabili Wakulima.
Ndikilo amesema kwamba
anashangazwa kuona kuna baadhi ya viongozi na Watendaji Wanashindwa
tutimiza Wajibu wao ipasavyo Na kuanza kukwepa Majukumu kwa Visingizio Ambavyo havina Tija, na kuamua kufanya Hujuma kwa kupinga Mfumo huo
kitu Ambacho amesema ni lazima atawashughulikia kikamilifu watu kama hao
ambao Hawataki kuleta Maendeleo kupitia Sekta ya kilimo.
No comments:
Post a Comment