Rais Dkt John Pombe Magufuli
Na Kalonga Kasati
Adhabu
inawanyemelea watumishi wa serikali Waliokaidi Agizo la kutosafiri nje
ya nchi bila kibali cha Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue.
Habari Zilizopatikana kutoka Baadhi ya Wizara zilieleza kuwa Tayari Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara Wameshapewa Orodha ya Majina ya Watumishi Waliosafiri Nje Ya nchi kinyemela.
Chanzo
kimoja cha habari kimesema kuwa tayari majina hayo yamepatikana na
kinachofanyika sasa ni kupitia taratibu, sheria na kanuni kabla ya
kuwachukulia hatua.
Watumishi
wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
wamesimamishwa kazi kwa kwenda nje ya nchi licha ya maombi yao ya
kusafiri kukataliwa na mamlaka.
Jana
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Dk.
Donald Mmbando alikiri kukabidhiwa taarifa kuhusu Watumishi waliosafiri
nje ya nchi bila kibali cha Ikulu na kwamba kwa sasa kuna Taratibu
ambazo zinafanyiwa kazi na ngazi Husika kwa ajili ya kuchukua hatua
zaidi.
“Ni
kweli niliagiza Nipatiwe Taarifa ya Watumishi Hao na Nimeshapewa ila
kuna Taratibu Ambazo zinafanyiwa kazi na zitakapokamilika itatolewa Taarifa ya wale wote Waliosafiri na Wamefanywa nini,” Alisema Dk. Mmbando.
“Kwa Sasa Siwezi kulizungumzia ila likikamilika Tutawajulisha.” Hivi
karibuni Dk. Mmbando Alitoa Taarifa kwa Wakuu wa Idara wizarani kwake Akiwataka ifikapo Desemba 21 Awe Amepata Taarifa ya Wale Wote Waliokiuka Agizo la Rais la kutosafiri nje ya Nchi.
Dk.
Mmbando Aliandika Dokezo kwenda kwa Wakuu wa idara hiyo Ambayo
iliwataka kuwataja Watumishi Walio chini yao Ambao Walisafiri nje ya
nchi Baada ya katazo la Rais Dk. Magufuli.
Katika Dokezo hilo Walitakiwa kueleza Watumishi hao wamesafiri kuelekea nchi
gani, Tarehe ya safari, madhumuni ya safari hizo, Safari hizo
zimegharamiwa na nani pamoja na kiasi cha fedha kilichotumika.
Waliosimamishwa kazi Takukuru ni Msemaji Doreen Kapwani, Mary Mosha, Ekwabi Mujungu na Rukia Nikitas.
Awali,
Ofisi ya Rais ilisambaza mwongozo kwa Taasisi na Mashirika ya Umma Unaoweka Masharti ya ambayo Watumishi wa umma Wanaotaka kusafiri Nje ya
nchi Watatakiwa kuyatimiza ili Wapewe kibali cha kusafiri.
Masharti
hayo ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi Sefue na Maombi Hayo Yawasilishwe kwa Msajili wa Hazina kabla ya kwenda kwa Sefue ili Mwombaji Aweze kujenga Hoja kwa kuzingatia Umuhimu wa Safari hiyo na Tija itakayopatikana kutokana Na Safari hiyo.
Masharti
hayo Yanamtaka Mtendaji Mkuu wa Shirika ama Taasisi Apime Aonekane kama Safari Hiyo ni Muhimu kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi kabla ya
kuwasilishwa Hazina.
Sharti
lingine ni Umuhimu wa safari hiyo na isipofanyika itaathiri vipi Taifa
na Mwombaji Aeleze Manufaa ya Safari hiyo kwa taasisi na Taifa kama
imewahi kufanyika Huko Nyuma.
Ofisi
za Umma zilipokea barua kutoka kwa Msajili wa Hazina Novemba 12 Mwaka
huu ikieleza kuwa Rais Magufuli Ametoa zuio la Jumla kwa Safari za nje
ya nchi katika Utumishi Wote wa Umma na Mihimili yake. Barua Hiyo ya
Hazina ilisema zuio hilo litadumu Hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.
No comments:
Post a Comment