Muonekano
wa Moja ya Majengo ya Hospitali Ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Itakayohudumia Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma Inayojengwa eneo la
Mikindani Mkoani Mtwara.
UJENZI wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini, unaofanyika Mkoani Mtwara Sasa upo katika Majengo ya Wagonjwa wa nje (OPD).
Ujenzi huo Ulioanza Mwaka 2009 kwa kusafishwa kwa eneo na kujengwa kwa Uzio wa
kilomita 2.7 mwaka 2011 kwa Gharama ya Shilingi Milioni 840 na kuanza
kujengwa kwa Majengo ya OPD mwaka 2013 Umelenga kuwezesha Mikoa ya
Kusini kuwa na Hospitali kubwa yenye Hadhi ya kisasa.
Akisoma Taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi kwa Naibu Waziri katika Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla,
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Alisema kwamba Ujenzi wa Mapokezi Umetarajiwa kutumia Sh.bilioni 4.8 na hadi Sasa Wametumia Bilioni 1.8
Mganga huyo alisema Mradi Mzima Unatarajiwa kujengwa kwa Bilioni 78.
Alisema
kuchelewa kuendelea Japo Sasa wana Ghorofa 2 Zilizoezekwa na Wanapiga
ripu kunatokana na Upatikanaji wa fedha kutoka Serikali kuu.
Alisema Hospitali Hiyo ni Muhimu Sana kukamilika kutokana na kukua kwa Uchumi wa
Mtwara na Mikoa Jirani na pia kuwapo kwa Uhitaji kwa mikoa ya kaskazini Mwa nchi jirani.
Naye Naibu
Waziri Kigwangwalla alisema kwamba ni Matumaini yake kuwa Hospitali hiyo
itakamilika Mapema na kubakiza Changamoto za Matumizi ya Wananchi
kutoka nchi Jirani ambao kwa Sasa Wanafaidika Sana na Hospitali ya
Ligula.
Alisema
wataalamu wanatakiwa kuangalia Hali Hiyo ili kuwepo na Matumizi Sahihi
ya Miundombinu hiyo iliyolenga kufaidisha Wananchi wa Tanzania.
Aidha akiwa Mtwara Naibu Waziri huyo Aliendelea kusisitiza Watumishi Wote kuwajibika Na kuwahi Maeneo yao ya kazi.
Alisema
watumishi wa Umma Wanaofikia laki nne Wamepata Nafasi adimu ya
kuutumikia Umma wa Watu takribani Milioni 50 na Hivyo ni lazima Waheshimu Watanzania kwa kuwatumikia Ipasavyo.
Alisema wao Waliomba Nafasi ya kuhudumia Watanzania kwa hiyo ni lazima wawahudumie Watanzania na kila Mmoja katika kitengo chake ni lazima kuhakikisha Watumishi Wanafanya kile Walichoahidi katika Mikataba yao.
.
No comments:
Post a Comment