Saturday, 19 December 2015

Tume Ya Uchaguzi Yatangaza Majimbo ya Uchanguzi kesho Yaliokuwa Yamesalia Kutokana na Wagombea kufariki Dunia

PICHA 3.Jaji  Lubuva (kushoto) akifafanua kuhusu Taarifa Aliyoitoa iliyohusu Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa, kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Wa Tume hiyo BwanaKailima Ramadhani.Picha Na Kalonga Kasati
 PICHA 4Baadhi ya Waandishi wa Habari Waliohudhuria Mkutano huo Wakifuatiliana Taarifa ikiyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kuhusu Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa.Picha Na Kalonga Kasati
 PICHA 6Lubuva (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwana Kailima Ramadhani wakijadili Jambo Mara Baada ya kutolewa kwa Tarifa ya Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa

Na Kalonga Kasati

Majimbo ya Masasi Mjini Mkoani Mtwara na Ludewa mkoani Njombe yanatarajia kufanya Uchaguzi wa wabunge kesho (20.12.2015) ili kuwapata viongozi Watakaoongoza Majimbo hayo kwa kipindi cha Miaka Mitano.

Majimbo hayo hayakufanya uchaguzi tarehe 25.10.2015 kutokana na baadhi ya wagombea katika Majimbo hayo kufariki dunia.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji  Damiani Lubuva Amewasihi Wananchi kujitokeza Na kupiga kura kwa Amani na Utulivu. Jaji Lubuva Amesema Hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati Akiongea na Waandishi wa Habari.

“Tume Inawasihi na kuwashauri wananchi kujitokeza kupiga kura kwa amani. Hakuna Sababu Masasi na Ludewa kuwa Tofauti na Majimbo Mengine yaliyofanya Uchaguzi kwa Amani na Utulivu,” Alisema Lubuva.

Hata hivyo, Mwenyekiti Huyo Amewaonya      Viongozi wa Vyama vya Siasa kutoingilia kazi ya Tume katika Uchaguzi huo.

“Viongozi wa vyama vya Siasa Wasiingilie kazi ya Tume ya Uchaguzi. Ulimwengu Unatusifia kuwa Uchaguzi Uliopita Ulifanyika kwa amani. Kila Mwananchi, Viongozi wa Dini na vyama vya siasa Tushirikiane Wote kuhakikisha kuwa Viashiria vya Uvunjifu wa Amani na Utulivu Vinaepukwa ili Uchaguzi Uwe Huru, wazi na wa Haki,” aliongeza Lubuva.

Jaji Lubuva alisisitiza kuwa watu wakisha piga kura Waondoke vituoni ili kutowazuia Wananchi Wanaokuja kupiga kura isipokuwa Mawakala na Wasimamizi wa Uchaguzi Wanaoruhusiwa kwa Mujibu wa Sheria.

Kwa Mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Daftari la Wapiga Kura litakalotumika Ndio lile lililotumika Wakati wa Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Oktoba 25, 2015.

Baada ya Uchaguzi wa majimbo ya Ludewa na Masasi Mjini, litasalia Jimbo la Kijitopele Zanzibar ambalo Uchaguzi Wake utategemea lini Uchaguzi wa Zanzibar Utakapofanyika.

No comments:

Post a Comment