Msemaji wa Jeshi la polisi Advera Bulimba
Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 na
kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2016, Wananchi Hutumia Muda huo kwenda katika Nyumba za ibada Ama kusherekea katika Maeneo Mbalimbali ya Starehe, Ambapo Uzoefu Unaonyesha kuwa Baadhi Ya watu Hupenda kutumia fursa Hiyo
kufanya Vitendo Vinavyohatarisha Usalama wa Raia Mali zao.
Jeshi la Polisi nchini, limejipanga
vizuri katika Mikoa yote kwa kushirikiana na vyombo vingine Vya Ulinzi
na Usalama ili kuhakikisha kwamba Vitendo vyovyote vya Uhalifu
vitakavyojitokeza Hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mkesha Wa Mwaka Mpya vinadhibitiwa.
Ulinzi Umeimarishwa kwenye maeneo yote ya
kuabudia, Fukwe za Bahari, sehemu za starehe na Maeneo Mengine yote
ambayo yatakuwa na Mikusanyiko Mikubwa ya watu.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa Tahadhari
kwa Wananchi wote kuwa makini na kuchukua Hatua Stahiki za Haraka kwa
kutoa Taarifa Pindi Wanapoona Viashiria vyovyote vya Uhalifu katika Maeneo yao ya Makazi ama Maeneo ya Biashara. Simu za polisi Endapo Mwananchi atakuwa na Taarifa ni 111 au 112.
Pia, Jeshi la Polisi linawatahadharisha Wale wote Ambao watakuwa wakitumia Barabara kuwa Makini na kuzingatia
sheria za Usalama Barabarani Na Hasa kwa Madereva wa Magari na Pikipiki,
kuepuka kujaza Watu kupita kiasi, kwenda Mwendo kasi, kutumia vilevi
pamoja na kupiga Honi ovyo.
Vilevile, Wananchi kuacha Tabia ya
kuchoma Matairi Barabani Pamoja na kupiga Mafataki. Aidha, Yeyote
atakayefanya Vitendo Hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa Dhidi
yake.
Nawatakieni Watanzania Wote kheri ya Mwaka Mpya.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment