


Baada ya Taflani iliyotokea Jana
Jumatatu kati ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea wa Chadema na Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Eneo la Viwanda (EPZA) Mabibo jijini
Dar hali Iliyopelekea DC Makonda kuwaamuru Polisi Wamuweke Chini ya Ulinzi Saed Kubenea na kumpeleka Kituo cha Polisi.
Leo Saed Kubenea amepandishwa
kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam
na kusomewa Shitaka la kutoa lugha Chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda.
Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya Kitendo Hicho na kesi yake Kuahirishwa hadi Disemba 29, Mwaka huu huku Uchunguzi Ukiendelea.
No comments:
Post a Comment