Mwanasheria Mkuu Mstafu wa Serikali, Jaji Mark Bomani amelaani Vitendo vya Mauaji dhidi ya Watu na Mifugo
Akizungumza na Wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani Amesema kuwa hivi karibuni kumejitokeza Wimbi la Vikundi vya Watu Vinavyofanya Vitendo vya Ukatili Hususani Upande Wa Wafugaji na Wakulima kugombania Mashamba na Hatimaye kuuana na kuua Mifugo.
Bomani amesema Zaidi ya ng’ombe 70 hivi Majuzi Waliuawa na watu kadhaa Wakajeruhiwa Huko Mvomero, Morogoro, kutokana na Migogoro ya Wakulima na Wafugaji, Jambo ambalo linabidi Kudhibitiwa lisiendelee kujitokeza kwenye jamii.
Aidha amesema Miongoni Mwa Makundi hayo yamekuwa yakiharibu Mimea kwa kuikata na kuichoma Zikiwemo nyumba za wawekezaji Ambapo ameitaka Serikali kuchukua Hatua kali Dhidi ya Vitendo hivyo.
Vilevile amesema Serikali inapaswa kuweka Vipaumbele vya hali ya Juu katika kuhakikisha inatatua Migogoro iliyopo baina ya Wafugaji na Wakulima kwenye Jamii husika ili kupunguza Vitendo vya kikatili Vinavyoendelea kushamiri.
No comments:
Post a Comment