Upelelezi
wa kesi ya Uhujumu Uchumi Ulioisababishia Serikali Hasara ya Sh bilioni
12.7 inayomkabili Aliyekuwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Mamlaka ya
Mapato (TRA), Tiagi Masamaki na Wenzake, Haujakamilika.
Wakili
wa Serikali, Diana Lukondo alidai Hayo jana katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa. Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama
hiyo, Huruma Shaidi Aliahirisha kesi Hiyo Hadi Januari 13 Mwakani
itakapotajwa Tena.
Mbali
na Masamaki Washitakiwa wengine katika kesi Hiyo ni Vigogo Wengine wa Mamlaka hiyo, Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja TRA, Habibu Mponezya,
Meneja Udhibiti wa Forodha na Ufuatiliaji, Burton Mponezya, Mchambuzi
Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamisi Omary (48) na Haroun
Mpande wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta TRA.
Wengine
ni Wafanyakazi wa Bandari Kavu (ICD) ya Azam, Msimamizi Mkuu Kitengo
cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema (31), Meneja wa Oparesheni
za Usalama na Ulinzi ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam
ICD, Ashraf Khan (59).
Washitakiwa Saba Wameachiwa kwa Dhamana Huku Mpande Akiendelea kusota Rumande Baada
ya kushindwa kutimiza Masharti ya Dhamana. Masamaki, Habib Mponezya na
Burton Mponezya wao Waliachiwa Huru kwa Dhamana.
Wanadaiwa
katika Tarehe Tofauti kati ya Juni Mosi na Novemba 17, Mwaka huu sehemu
isiyofahamika, walikula njama za kuidanganya Serikali kuhusu Sh Bilioni
12.7, kwa Madai kuwa Makontena 329 Yaliyokuwa kwenye ICD ya Azam Yametolewa Baada ya kodi zote kufanyika, Jambo Ambalo si kweli.
No comments:
Post a Comment