Na Kalonga kasati
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John pombe
magufuli amevunja bodi ya bandari nchini pamoja na kutengua uteuzi wa katibu
mkuu wa wizara ya uchukuzi Dk Shabani Mwinjaka pamoja na Mkurugenzi mkuu wa bandari Awadhi
massawe na mwenyekiti wa bodi ya bandari
Profesa Joseph msambichaka
Kuvunjwa kwa bodi hiyo kumetokana na uendaji mbovu wa
mamlaka hiyo kwa muda mrefu na kitendo cha kutokuchua hatua za haraka katika
vyanzo husika.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
waziri mkuu Kassim majaliwa ofisini kwake leo jijini Dar es salaam amesema
kutenguliwa kwa uteuzi huo kutokana na ziara alizofanya bandari ya Dar es
salaam na kubaini kuwepo na mianya ya
ukwepaji wa kodi ikiwemo makontena 2387 yaliyopitishwa kati ya machi na
septemba mwaka jana.
Amesema upotevu huo kutokana na mfumo wa kupokelea
malipo ambao unatoa mwanya wa kupoteza mapato ya serikali kutaka mfumo huo
ubadilishwe kufikia desemba 11.
Waziri mkuu kassim majaliwa amesema kuwa kutokana na
utendaji wa bandari huo mbovu iliwataja majina ya wahusika na upitishaji wa
makontena hayo bila ya kuwepo na taarifa yoyote hivyo amewasimamisha kazi
wasimamizi 8 wa bandari kavu (icd) ambao ni Happy god Naftari juma Prosper
kimaro mkango ali John Elisante na James Kamwomwa.
Wengine ambao hakuwepo kwenye ripoti hiyo ni viongozi
wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari wahusika wakuu hao
ni Shaban mngazija aliyekuwa meneja mapato Rajab mdoe Mkurugenzi wa fedha na mkuu wa bandari kavu ibin masoud kaimu
mkurugenzi wa fedha Apolonia mosha meneja wa bandari msaidizi wa fedha
Na kalonga kasati
Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma nchini
ambao ulizinduliwa agosti mwaka huu
Akiongea na vyombo vya habari leo katibu mkuu Hab
mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi disemba 2015 ambapo kila mtumishi
wa ummaataweka saini ya kiapo kwa kuzingatia taratibu zilozoweka na mazingira
ya taasisi husika
Utaratibu wa utekelezaji wa ahadi ya uadilifu kwa
utumishi wa umma umetolewa kupitia waraka wa mkuu wa utumishi wa umma wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa ahadi ya
uadilifu kwa viongozi watumishi wa umma wa sekta binafsi wa tarehe 1 agosti
2015 alisema mkwizu.
Mkwizu aliongezea kwa kusema uanzilishwaji wa uadilifu
ni mwendelezo wa uundaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko
kubwa la ubadhirifu utoro sehemu za kazi kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha
miaka ya thelathini na tisini
Alivitaja vyombo vipengele ambavyo vilianzishwa
kusimamia ahadi kuwa ni sektarieti ya maadili ya viongozi wa umma tume ya haki
binadamu na utawala bora na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)
Aidha Mkwizu amtoa kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa
utekelezaji wa ahadi ya uadilifu unakamilika ifikapo tarehe 31-12-2015 na
utekelezaji wakekwa kila ifikapo juni 30 ya kila mwaka fomu ya ahadi ya
uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Rais.
No comments:
Post a Comment