Monday, 21 December 2015

Waziri Kitwanga AKutana na Waandishi wa Habari Leo na Kuongelea Kuhusu Madawa Ya Kulevya


Waziri Kitwanga Akizungumza na Waandishi Wa Habari
Na Kalonga Kasati

Leo Waziri wa Mambo ya ndani Charles Kitwanga leo amekutana na waandishi wa Habari Dar es salaam.

Baada ya kufanya ziara katika maeneo Mbalimbali ya ofisi za Jeshi la Polisi kikubwa Alichozungumza ni kuhusu Ugaidi, Ubambikaji kesi kwa Wananchi, Matumizi ya TEHAMA pamoja na Madawa ya kulevya.

Mikakati ya kupambana na dawa za kulevya hapa nchini..“Nimepata Maelezo ya kutosha kuhusu kinachoendelea…kitakachotusaidia  ni lazima Tuwe na Mfumo mzuri wa kuhakikisha Madawa ya kulevya hayaingii katika nchi yetu, kwangu orodha ya wahusika hainisadii, kinachosaidia ni kuhakikisha madawa Hayaingii na yale yaliyopo yanatafutwa na kukamatwa na wahusika wanafikishwa katika vyombo husika”..Charles Kitwanga.

“Tumekubaliana Tutaanza Utekelezaji wa Mara moja, kuhakikisha Tunaongeza Nguvu kuhakikisha mfumo mzima wa usambazaji na uingizaji tunauvunja”.

Askari Polisi kukosekana katika bandari ya Dar es salaam...”Tumelijadili na tutajadiliana na wenzetu tuone ni utaratibu gani utatuwezesha kuhakikisha bandari yetu inakuwa salama, kama kuna askari amekosea anachukuliwa hatua na si kuvunja mfumo mzima”…

Ubambikaji kesi wananchi..“Tumelijadili na Wenzangu Polisi Wamejipanga vizuri kuhakikisha kwamba kabla ya mashtaka Tuhakikishe kwamba mtu aliyekamatwa Ashtakiwe kwa kosa alilolifanya na si kupewa Makosa ya kufikirika” na hili Tutashirikiana na Wenzetu wa Sheria na katiba”.. .

Msongamano wa Magari Dar es salaam na kwingineko..“Tutaboresha zaidi ili kuhakikisha Haya Malalamiko ya Wanannchi yanakuwa Hayapo”.

Matumizi ya TEHAMA...”Matumizi ya Teknolojia ndani ya jeshi ikiwemo CCTV, Matumizi ya kusajili magari, leseni, ulipaji faini kwa kutumia Tehama..Haya tumeyajadili na Yote yatafanyiwa kazi kwa wakati mmoja kisha kutolewa ufafanuzi…Charles Kitwanga

Idadi ya askari waliopo na Mikakati ya kuwapati makazi...”Tuna idadi ya Askari 45,000 ambao bado hawatoshi, wanaokaa katika nyumba za Polisi ni kama 10,000 tu, Tuna upungufu wa nyumba kama 35,000, Tuna mpango wa kujenga nyumba nyingine kama 5,000, tutajenga polepole kuligana na uwezo Wetu, nia ni kuhakikisha  Askari wote wanakaa sehemu moja ili kurahisisha ufanyaji kazi”..

No comments:

Post a Comment