Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Akisalimiana na watendaji Mbalimbali wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Waliofika Katika kituo cha Feri cha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) leo Jijini Dar es Salaam. Picha Na Kalonga Kasati
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Akitembelea Maeneo Mbalimbali ya kituo cha Feri jijini Dar es Salaam leo.Picha Na Kalonga Kasati
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Majaliwa Akipanda basi la Mwendo wa Haraka mara Baada ya kutembelea Maeneo Mbalimbali katika kituo cha feri leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa Akiwa
katika kituo cha Mradi wa Mabasi cha Jangwani kukagua Maendeleo ya Ujenzi ya kituo hicho ikiwa Ujenzi wa kituo hicho upo Hatua za Mwisho
kukamilika.
Kituo cha Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kikiwa kimekamilika na Mabasi yakiwa Nyuma ya kituo Hiki kwaajili
yakisubiri kumalizika kwa barabara ili ifikapo Januari 10, 2016 kuanza
kufanya kazi.Picha Na Kalonga Kasati
Mabasi ya Mwendo wa Haraka yakiwa kwenye Maegesho.
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa Majaliwa Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es
Salaam leo Mara baada ya kumalizia kukagua Ujenzi wa Barabara ya Mradi
wa Mabasi yaendayo Haraka katika kituo cha Morocco jijini Dar es Salaam.
Na kalonga Kasati
MRADI wa Mabasi
yaendayo kasi (BRT) kuanza Januari 10, 2016 hayo yamesemwa na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa wakati Akikagua Ujenzi wa Miundo mbinu ya
Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka leo jijini Dar es Salaam.
Pia Majaliwa Amewaagiza Watendaji wizara ya
Tamisemi Ambao ni Wamiliki wa Mradi Huo kusimamia Vyema ili Uanze
kufanya kazi kama ilivyo pangwa kwa kuwa Mabasi 120 Yalishawasili
jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Ameanza kwa kukagua vituo vya Mradi Huo kuanzia cha Feri, Jangwani, Kimara na kumalizia na Morocco na
kuwapongeza kwa kumaliza kujenga Vituo 15 kati ya 27 na Amewaagiza
kumalizia vituo Vilivyo baki ili kufikia januari 10 Mwakani Mabasi
yaanze kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment