Thursday, 31 December 2015

Jeshi la Polisi latoa Onyo Kali Watakaovunja Amani Ya Raia na Mali zao


Msemaji wa Jeshi la polisi Advera Bulimba


Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2016, Wananchi Hutumia Muda huo kwenda katika Nyumba za ibada Ama kusherekea katika Maeneo Mbalimbali ya Starehe, Ambapo Uzoefu Unaonyesha kuwa Baadhi Ya watu Hupenda kutumia fursa Hiyo kufanya Vitendo Vinavyohatarisha Usalama wa Raia Mali zao.

Jeshi la Polisi nchini, limejipanga vizuri katika Mikoa yote kwa kushirikiana na vyombo vingine Vya Ulinzi na Usalama ili kuhakikisha kwamba Vitendo vyovyote vya Uhalifu vitakavyojitokeza Hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mkesha Wa Mwaka Mpya vinadhibitiwa.
 Ulinzi Umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, Fukwe za Bahari, sehemu za starehe na Maeneo Mengine yote ambayo yatakuwa na Mikusanyiko Mikubwa ya watu.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa Tahadhari kwa Wananchi wote kuwa makini na kuchukua Hatua Stahiki za Haraka kwa kutoa Taarifa Pindi Wanapoona Viashiria vyovyote vya Uhalifu katika Maeneo yao ya Makazi ama Maeneo ya Biashara. Simu za polisi Endapo Mwananchi atakuwa na Taarifa ni 111 au 112.


Pia, Jeshi la Polisi linawatahadharisha Wale wote Ambao watakuwa wakitumia Barabara kuwa Makini na kuzingatia sheria za Usalama Barabarani Na Hasa kwa Madereva wa Magari na Pikipiki, kuepuka kujaza Watu kupita kiasi, kwenda Mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga Honi ovyo.


Vilevile, Wananchi kuacha Tabia ya kuchoma Matairi Barabani Pamoja na kupiga Mafataki. Aidha, Yeyote atakayefanya Vitendo Hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa Dhidi yake.

Nawatakieni Watanzania Wote kheri ya Mwaka Mpya.

Imetolewa na: Advera John Bulimba-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.

2016 Mwaka wa Matumaini Kwa Watanzania

 
Rais John Pombe Magufuli

 Na Kalonga Kasati
Mwaka 2016 ni Mwaka wa Matumaini Mapya kwa Watanzania wWote Walioanza kukata Tamaa ya Maisha Bora. Biashara nyingi Zimefilisika kutokana na vikwazo Mbalimbali.

Familia nyingi Zimeparaganyika kutokana na kukithiri kwa Mmomonyoko wa Maadili ya kitaifa na kunyauka kwa Utu wa Ubinadamu Uliochochewa na Hali Duni ya Maisha Miongoni mwa Jamii.

Watu Masikini na wenye kipato cha chini Wameendelea kukosa mtetezi.

Mwaka 2015, wazee wenye umri zaidi ya Miaka 65, ambao hawazidi milioni mbili na Nusu hapa nchini, kwa muda mrefu walipaza kilio chao kuhusu haki yao ya msingi ya kupata ‘mrejesho wa hifadhi ya Jamii baada ya kulitumikia Taifa lao kwa zaidi ya miongo sita, lakini hakuna aliyewasikiliza.

Huduma za afya ya msingi zilizidi kuwa duni Zaidi katika Hospitali na vituo mbalimbali vya Afya nchini. Kiwango Duni cha Elimu na Mitalaa iliyopoteza Mwelekeo, ni Baadhi ya vizingiti vilivyoikwaza Sekta ya elimu.

Ile dhana ya kikoloni ya kuwalipa Wafanyakazi Ujira mdogo au Mishahara kiduchu au ya kiwango cha chini isiyozingatia utu wa Binadamu, iliendelea kukumbatiwa na Awamu zilizotangulia.

Kutokana na haya yote, siyo Jambo la Ajabu , kuikuta Tanzania ikishika nafasi ya 151 Miongoni mwa nchi 170 Duniani, kwa kiwango Cha chini cha hali ya Ubora wa Maisha ya Watu wake.

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) , katika Ripoti yake ya Mwaka 2015 , iliyotoa Matokeo ya Tathmini za uUtafiti Uliofanyika katika nchi Wanachama, ilidhihirisha Wazi jinsi Ambavyo Hata nchi Zenye kipato kikubwa zilivyoshindwa kutumia Utajiri wake ili kuboresha hali ya maisha ya Watu wake.

Utafiti huo uliangazia katika Maeneo Makuu Matatu; huduma za Afya, ubora wa elimu na viwango vya Mapato.

Nchi nyingi zilizojikuta katika kundi la nchi Zenye kiwango cha chini cha Ubora wa Hali ya Maisha ya Watu wake, zilitoka Bara la Afrika, Baadhi yake zikiwa na Utajiri Mkubwa wa Maliasili na Rasilimali.

Katika kundi hilo, Kenya ilionekana kuwa na Unafuu zaidi kwa kupata kiwango cha 0.548 (HDI) na kuongoza kundi hilo lenye nchi 44.

Nchi iliyoshika mkia katika kundi hilo ni Niger, iliyopata kiwango cha 0.348 , ikilinganishwa na Viwango vya juu vilivyoshikwa na nchi ya Norway (HDI 0.944) na Mauritius iliyoongoza katika nchi za bara la Afrika kwa kiwango cha HDI 0.777.

Ripoti hiyo inabainisha pia kwamba katika Miaka 25 iliyopita, karibu watu wapatao Bilioni Mbili kutoka nchi mbalimbali, walifanikiwa kujinasua kutoka katika kundi la nchi zenye kiwango cha chini cha ubora wa Hali ya Maisha.

Tanzania yenye watu wapatao milioni 45, kuendelea kubaki katika kundi la nchi 44 Zenye kiwango cha chini cha ubora wa hali ya Maisha ya watu wake, ni kiashiria cha wazi cha kushindwa kwa sera, mifumo na mikakati Yake ya matumizi sahihi na makini ya maliasili Na Rasilimali zake

Kwa Mtazamo mwingine ni kwamba, Tanzania ilishindwa kuwa sehemu ya nchi hizo zenye Watu Bilioni Mbili waliofanikiwa kujinasua kutoka katika kundi hilo la Ubora wa chini.

Mwaka 2016

 Yapo Mikononi Mwa Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Kila Mtanzania Anatarajia labda Uongozi huu Utakuja na kitu kipya katika maisha yao, Ambacho kilisahaulika kwa Miaka Mingi. Nacho ni kutokomeza Ufukara na umasikini wa kipato kwa vitendo.

Kama Miaka 25 iliyopita Tumeipoteza Bila ya kufikia Malengo tuliojiwekea, kutokana na Sababu Mbalimbali, Tatuna sababu Tena ya kupoteza Miaka Mingine 25 ijayo.

Hata hivyo, Uongozi mpya wa Awamu ya Tano, Umeanza kuonyesha Dalili Njema za kukabiliana na adha hiyo.

Serikali ya sasa imerithi Uchumi ukiwa katika Hali Duni na tegemezi, huku Taasisi nyingi za Umma au za Serikali zikiwa hazifanyi vizuri kama ilivyo kusudiwa. Rushwa na ufisadi Navyo vimetapakaa katika kila nyanja ya Maisha yetu.

Yote hayo yanafanyika Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi chache Barani Afrika zilizobahatika kuwa na utajiri mkubwa wa Maliasili na Rasilimali Mbalimbali.

Mtu yeyote aliye na Dhamira ya kufunga Safari, Tena safari Ndefu, kwanza lazima ajue Wapi Anakotaka kwenda. Akisha jua wapi Anakotaka kwenda, Pili, lazima ajue njia Atakayopita na Namna ya kumfikisha huko Alikokusudia kwenda

Uongozi Mpya wa Awamu ya Tano, Utalazimika kuangalia Nyuma Tulikotoka (miaka 25 iliyopita). Kisha Utafakari, Tunaitaka Tanzania ya aina Gani Miaka 25 ijayo?

Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Mahiga Ampokea Balozi Mteule Wa Palestina


Waziri wa Ushirikiano Wa kimataifa Augustine Mahiga Akiwa na Balozi Mteule Wa Palestina . Hazem Shabat

Taasisi za Dini zatakiwa kuwasilisha Nyaraka kwa ajili ya kuhakiki Ushuru Bandarini

Na Kalonga Kasati
Mashirika ya Dini ni Miongoni mwa Taasisi zilizotakiwa kuwasilisha Nyaraka kwa Ajili ya kuhakiki kama yalilipa Ushuru wa Bandari Uliosababisha Serikali kupoteza Sh48 Bilioni.


Uwapo wa Taasisi hizo za kiimani kwenye Sakata Hilo Ulibainishwa jana katika orodha ya iliyotangazwa Jana na Mamlaka ya Bandari (TPA) ambayo ina kampuni na Taasisi 40 zaidi ya orodha iliyotangazwa Juzi yenye kampuni 243. Kwa Tangazo la Jana, kampuni na Taasisi Zinazotakiwa kuwasilisha Nyaraka kuhusu Malipo Hayo Sasa ni 283.


Tangazo la TPA lilitolewa Jana likiwa na Tarehe ya Desemba 24, linazitaka Taasisi hizo Ambazo ni Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki, Caritas Tanzania na Nyingine 281 kwenda kuchukua Barua zao kwa Ajili ya Uhakiki wa Malipo ya Ushuru huo yaliyofanyika kuanzia Julai 2014 hadi Aprili, 2015.


Taasisi Nyingine Maarufu zilizopo katika orodha hiyo ni klabu Maarufu ya Mchezo wa Soka ya Azam Football, kampuni Maarufu ya Toyota Tanzania Ltd na Bakhresa Food Products.


Juzi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa Alizihusisha baadhi ya taasisi hizo 283 na Upitishaji wa makontena 11,884 na magari 2,019 kwenye bandari bila kulipia ushuru wa Bandari.


 Kubainika kwa Ukwepaji Huo Ushuru, kunafanya idadi ya Makontena yaliyohusika katika Suala hilo kufikia 14,664. Awali Makontena 349 yaligundulika kupitishwa kinyemela Baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufanya ziara Bandarini na Mengine 2,431 kubainika Baadaye.


Mbarawa aliwataka Mawakala wa forodha na kampuni hizo 283 zinazotuhumiwa katika Utoaji wa makotena na Magari Bila kulipia Ushuru kupeleka Vielelezo vya Uthibitisho Ndani ya siku saba kuanzia juzi.


Msemaji wa CCT, Mchungaji John Kamoyo Alisema Watafanya kama lilivyoagiza kwenda kuchukua Barua zao.



“Kama Walivyoeleza sisi Tutaenda kuchukua Barua na kufahamu kilichopo ndani na Tutafanya kama Walivyoagiza,” Alisema Kamoyo Huku akikataa kuhusisha wito huo na suala lolote linalohusina na ukwepaji wa kodi.


Katibu Mtendaji wa Caritas Tanzania, Laurent Masui Alisema Atashirikiana na Mamlaka hiyo kutimiza Agizo hilo.

“Ni kweli Tunahusika na Utoaji Mizigo Bandarini lakini kwa Wateja Mahususi kutoka Mashirika Ya kidini Ambayo Husamehewa Baadhi ya kodi Na Ushuru. 
 Lakini Tozo Nyingine huwa Tunalipa na kwa kuwa Tangazo lenyewe linaonekana ni  kiutawala, basi Nitawatuma Maofisa wangu Haraka wafuatilie ili Tujue kama Tulizidisha Ushuru au Tulitoa Pungufu,” alisema.   Nasui  

Kova kukoma leo kufanya kazi




Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Suleiman Kova.

 Na Kalonga Kasati

Leo ni Siku ya Mwisho kwa Kamanda wa kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova, kulitumika jeshi la Polisi nchini kwa kuwa Muda Wake wa kulifanyia kazi Jeshi hilo Umeisha.

Kamanda Kova Ametoa Taarifa Hiyo leo Asubuhi Alipokuwa Akizungumza katika kipindi cha kumekucha cha ITV, na kusema kuwa Mkataba Wake na Jeshi la Polisi umeishia leo, hivyo Analazimika kukaa pembeni.


“Mmepata bahati sana, maana wakati Nakuja Dar es Salaam mwaka 2008 Nikitokea Mbeya, kwa mara Ya kwanza nilifanya kipindi Hapa na leo Hii Nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, Mkataba Wangu na Jeshi la Polisi Unaisha leo, lakini Siwaachi Hivi hivi, Kaimu wangu yupo Atakuwa Nanyi”, alisema Kamanda Kova.


Kamanda Kova Alikuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, na kwa Mujibu wake Amefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa Matukio ya kiuhalifu, Yaliyokuwa yanaitikisa Nchi Hususani matukio ya wizi na uvamizi wa kwenye Benki.

Wednesday, 30 December 2015

NAPE: 60% ya Muziki Utakaochezwa katika Vyombo vya Habari lazima Uwe wa Nyumbani




Image result for nape nnauye
Nape Nnauye Waziri wa Habari na Utamaduni na Michezo Akizungumza na Waandishi wa Habari
Na Kalonga Kasati
Wakati Baadhi ya wasanii na wadau Mbalimbali wa Burudani nchini wakiendelea kuwa na Hofu Juu ya Mfumo mpya unaovitaka vituo vya redio na Runinga kuwalipa wasanii Mirahaba inayotokana na kucheza kazi zao, Serikali imesema imeunda sheria ambayo itavifanya Vishindwe kuepuka kucheza nyimbo za Wasanii wa Ndani.


Akizungumza  kwenye Uzinduzi wa filamu ya ‘Home Coming’ Mlimani City jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Nape Moses Nnauye alisema Sheria hiyo inazitaka TV na Redio zenye Vipindi vya Burudani kuhakikisha 60% ya Content ni ya Nyumbani.


“Tumeshatangaza kuanzia Tarehe Moja Mwezi wa kwanza 2016 kila Muziki wa msanii Utakaopigwa kwenye Redio ma Television Utalipiwa.


"Sheria ilishasainiwa na Tumekubaliana na Watu wa COSOTA Wataisimamia na Tumeweka kampuni ya kusimamia Muziki Umepiga mara ngapi na TV gani.


“Mimi Nataka Watu Waniamini Historia yangu, Waamini watu Watalipwa na Haki yao Wataipata Na Jasho lao watalipata. Nilichowaambia kila Jambo Jipya lazima litakuwa na mapungufu ila Sheria ndio Zitatuongoza, kila Redio na TV Zenye vipindi vya Burudani Wanatakiwa kuhakikisha 60% ya Content wanayoitoa iwe ya Nyumbani, Hakuna Wakukwepa hili,” Alisisitiza Nape.


Pia Nape alisema Tayari ameshakaa na Wahusika wa Vyombo vya Habari na kuzungumzia Namna ya Utekelezaji wa Suala Hilo.


“Vyombo vya Habari ndio Wamekuwa Wakinisukuma kufanya Hivyo, kwahiyo kama Wao ndio wWameamua Hivyo sisi Ulikuwa ni Utekelezaji na naamini kila kitu kitaenda Sawa.”

Kesi ya Wafanyakazi Wa TRA kusikilizwa Januari 13 Mwakani




Upelelezi wa kesi ya Uhujumu Uchumi Ulioisababishia Serikali Hasara ya Sh bilioni 12.7 inayomkabili Aliyekuwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Tiagi Masamaki na Wenzake, Haujakamilika.


Wakili wa Serikali, Diana Lukondo alidai Hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa. Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi Aliahirisha kesi Hiyo Hadi Januari 13 Mwakani itakapotajwa Tena.


Mbali na Masamaki Washitakiwa wengine katika kesi Hiyo ni Vigogo Wengine wa Mamlaka hiyo, Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja TRA, Habibu Mponezya, Meneja Udhibiti wa Forodha na Ufuatiliaji, Burton Mponezya, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamisi Omary (48) na Haroun Mpande wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta TRA.


Wengine ni Wafanyakazi wa Bandari Kavu (ICD) ya Azam, Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema (31), Meneja wa Oparesheni za Usalama na Ulinzi ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashraf Khan (59).


Washitakiwa Saba Wameachiwa kwa Dhamana Huku Mpande Akiendelea kusota Rumande Baada ya kushindwa kutimiza Masharti ya Dhamana. Masamaki, Habib Mponezya na Burton Mponezya wao Waliachiwa Huru kwa Dhamana.


Wanadaiwa katika Tarehe Tofauti kati ya Juni Mosi na Novemba 17, Mwaka huu sehemu isiyofahamika, walikula njama za kuidanganya Serikali kuhusu Sh Bilioni 12.7, kwa Madai kuwa Makontena 329 Yaliyokuwa kwenye ICD ya Azam Yametolewa Baada ya kodi zote kufanyika, Jambo Ambalo si kweli.

Simba Hali Tete

Kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr, licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa anaweza kutimuliwa Ndani ya kikosi hicho na nafasi yake kupewa kocha Wa zamani wa Timu hiyo, Mserbia, Goran Kopunovic, ameibuka na kusema suala hilo wala Halimtishi hata kidogo.
Kopunovic Mserbia, Goran Kopunovic
Hivi karibuni kuliibuka Taarifa za ndani ya Simba zikisema Uongozi Umempa Muingereza huyo Michezo ya Mzunguko wa kwanza iliyobakia kuhakikisha anapata matokeo mazuri la sivyo Anaweza kuondolewa kukioongoza kikosi hicho.

Akizungumza na Fofam media , Kerr Amesema Anachojiamini ni kwamba kazi yake Anaifanya ipasavyo hivyo hata akitimuliwa ni kama Wanamuonea tu.


“Hilo suala la kuondolewa wala Halinitishi Hata kidogo, nimekuwa nikiifanya kazi yangu kwa Ufanisi lakini mazingira yanatunyima kufanikiwa Na kupata ushindi.


“Kabla ya mechi yetu na Mwadui Tulikua tukifanya Mazoezi kwenye uwanja mbovu ambao ni kama Sehemu ya malisho ya ng’ombe, kocha unatakiwa kuiandaa timu katika hali nzuri ili mpate matokeo Mazuri. Pia siku moja kabla ya mechi tulikwenda Uwanjani tukaukuta haupo katika kiwango kizuri.


“Binafsi Hata Mimi Matokeo haya yananiumiza, Mashabiki wengi kutoka Dar walikuja kutusapoti lakini wameondoka Vichwa chini, Baada ya Mchezo. Nilimuona Mwanadada akilia kwa Uchungu kisa Hatujapata Ushindi, hiyo inaonyesha ni Jinsi gani mashabiki Wanaumizwa na Matokeo Mabaya,” alisema Kerr.


Sare iliyoipata Simba, Juzi Jumamosi ni ya Tatu Mfululizo, ilianza kutoka sare ya 2-2 Dhidi ya Azam kisha ikaambulia 1-1 na Toto Africans.

Kampuni Za Simu Zimepigwa Faini kwa Kuwapa Ajira Wageni


Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amebaini kuwepo kwa Wafanyakazi wa kigeni, walioletwa na kampuni za simu za mkononi kufanya kazi Zinazoweza kufanywa na Watanzania ikiwemo kufunga meza na viti vya kukalia.

Aidha, amebaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Halotel, raia wa Vietnam, ambao wanaishi nchini bila kibali cha kazi wala cha kuishi. Mavunde Aliyabaini hayo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua vibali vya ajira kwa wageni, baada ya Tangazo lililotolewa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama.

Akiwa katika kampuni hiyo ya Halotel, Mavunde Alibaini kuwepo kwa Baadhi ya Mapungufu, ikiwemo Baadhi ya Wafanyakazi kutopewa Mikataba ya Ajira na wenye ajira kutopewa Nakala za mikataba yao.

Mavunde aliagiza viongozi wa kampuni hiyo, kuhakikisha kufikia leo wafanyakazi wote wanapewa mikataba huku nakala za mikataba hiyo, ikipelekwa ofisini kwake na pia kuwataka kulipa madeni ya wafanyakazi, hasa madereva, ya saa za ziada (overtime) haraka iwezekanavyo.

“Tumegundua kuwepo kwa mapungufu Mengi katika kampuni yenu, hii ni pamoja na Wafanyakazi wenu kutojiunga katika mifuko ya Hifadhi ya jamii na kumekuwa na Makato Ambayo hayapo kwa mujibu wa sheria za kazi.

"Lakini pia kuna Wageni ambao Wako katika Hii kampuni yenu, Wanafanya kazi ambazo Zinaweza kufanywa na Watanzania, kwa Mfano Huyu Anayefunga Viti, hii kazi inafanywa Na Vijana Wetu…kibali chake kinaisha kesho, Naagiza Asipewe kingine na Aondoke,” alisema Mavunde.

Aidha, alisema katika masuala ya usalama mahali pa kazi, pia kuna mapungufu mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi kutopewa mafunzo ya kukabiliana na majanga, vipimo vya afya na makosa mengine ambapo kwa mujibu wa sheria aliwatoza faini ya Sh milioni sita.

Hata hivyo, wakati akiendelea kutoa maagizo hayo, mmoja wa maofisa wa Ubalozi wa Vietnam, Mai Anh Thai aliingia katika ukumbi Wa Mkutano na kutaka kumkatisha Naibu Waziri kwa madai kuwa Hakufuata utaratibu.

Kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa Huko, ilimlazimu Mshauri wa kampuni hiyo Ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara Moja, kumshauri ofisa huyo taratibu za ukaguzi zilivyo.

Baada ya kutoka katika kampuni hiyo, Mavunde na maofisa wa Uhamiaji, Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana na askari walilazimika kufika katika nyumba ambayo iko Mikocheni, Ambako inasadikiwa kuwa wapo raia wengi wa Vietnam wanaoishi hapo, huku wengine Wakiwa hawana vibali vya kuishi wala vya kazi.

Walipofanya Msako katika Nyumba hiyo, Baadhi ya Raia hao Walijificha na kufanikiwa kumkamata Mtu ambaye Hakuwa na kibali chochote. Hata Hivyo, Mmoja wa Walinzi wa Nyumba hiyo alisema Raia Hao walikuwa Wengi, lakini Baadhi yao walitoroshwa Juzi Usiku.

Awali akiwa katika Kampuni ya Airtel, Mavunde aliwapiga faini ya Sh milioni nne kutokana na kuwepo na mapungufu Mbalimbali katika Masuala ya Usalama na Afya Mahali pa kazi, ambazo Wanapaswa kulipa Ndani ya siku 14.

Aidha, Aliwataka waajiri Nchini kote, kuhakikisha wanasimamia Sheria za kazi ili kujenga Nchi ambayo Haina Misuguano. Mavunde alionya kuwa Wanaobeza kuwa hiyo Ni ‘nguvu ya soda’, Wafute Jambo hilo, kwani kazi hiyo ni endelevu.

Tuesday, 29 December 2015

Serikali Kufanya Operasheni Nchi Nzima Ya Kukagua Vibali Vya Ajira Kwa Wageni

 Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge kazi vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama Akizungumza Sheria za kazi na Waandishi wa Habari
 Na Kalonga kasati
Serikali imeamua Muda Wowote kuanzia Mwezi huu kuanza Ukaguzi wa vibali vya Ajira za Wageni nchini, kufuatia Muda wa siku 14 kuisha uliotolewa na Serikali katika Tangazo la Utolewaji wa vibali vya kazi kwa wageni Nchini lililotiwa saini Desemba 14 Mwaka huu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Aiira, Vijana na Watu Wenye ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), Ambaye Aliwataka Waajiri wote nchini kwa Muda wa siku hizo Wawe wametekeleza Matakwa ya Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini Na. 1 ya Mwaka 2015.


“Katika Taarifa Tuliyoitoa Mwezi huu, Tuliwajulisha Waajiri wote Wenye Waajiriwa Wageni ambao wana vibali vya kazi za Muda (Carry on Temporary Assignment) na wale Wote Wasiokuwa na Vibali vya Ajira Vilivyotolewa na kamishna wa kazi Nchini Kuwa Wanatenda kosa. 


"Kamishna wa kazi Amepewa Mamlaka kutoa vibali vya Ajira kwa Wageni Wanaotaka kufanya kazi Nchini. Hivyo Hakuna Mamlaka Nyingine yoyote inayoruhusiwa kutoa vibali Vya Ajira kwa Wageni,” Amesema Mhagama.


Amesema hayo   Tarehe 29 Desemba, 2015, Jijini Dar es Salaam Wakati Akizungumza na kikosi Maalum kitakachoendesha Operasheni hiyo chenye Wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uhamiaji na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA), ikiwa lengo ni kufuatilia kama Agizo lililotolewa na Serikali limefuatwa na kuhakikisha Taratibu zinazopaswa kufuatwa katika Utoaji wa vibali vya Ajira zinazingatiwa.


“Serikali ilitoa Muda wa siku 14 kwa Waajiri Wote wawe Wametekeleza Matakwa ya Sheria Na. 1 ya mwaka 2015 Vinginevyo Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi Yao.” Alisitiza Mhagama.


Mwezi Machi, Mwaka huu Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini Na. 1 ya Mwaka 2015 (The Non-Citizens (Employment Regulation) Act)). 


Sheria hii imeanza kutumika rasmi tangu Tarehe 15 Septemba, 2015. Sheria hiyo inaanzisha Mamlaka Moja Yautoaji wa Vibali vya Ajira kwa Wageni na Mamlaka hiyo ni Kamishna wa Kazi. 




 Baadhi ya wajumbe wa kikosi maalum cha kukagua vibali vya Ajira za Wageni kutoka Idara ya Uhamiaji nchini na Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), Wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama , Wakati Walipokutana Naye Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu (kazi na Ajira), Eric Shitindi Akieleza jinsi operasheni ya Kukagua vibali vya Ajira za wageni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani) wakati Alipokutana na Wajumbe wa kikosi Maalum Cha kukagua vibali Hivyo Jijini Dar es Salaam Tarehe 29 Desemba, 2015.


Baadhi ya Wajumbe wa kikosi Maalum cha kukagua vibali vya Ajira za Wageni kutoka, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uhamiaji nchini Na Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb) (hayupo pichani), wakati walipokutana naye Jijini Dar es Salaam 

Ufisadi Wa Bilioni 48 Waibuliwa Bandarini Watu 7 Watiwa Mbaroni, 8 Wanasakwa na Jeshi la Polisi

 

Waziri Wa Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa

Na Kalonga Kasati

Serikali imepoteza Jumla ya Sh48.47bilioni Baada ya makontena 11,884 na Magari 2,019 kupitishwa Badarini Dar es Salaam Bila kulipiwa kodi.

Hata Hivyo, Jumla ya watu saba Wanashikiliwa na Wengine nane Wanatafutwa Na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na Ukwepaji kodi huo Uliolikosesha Taifa mapato. 

Akizungumza na Wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Amesema Ufisadi huo umebainika Baada ya Serikali kuzifanyia Ukaguzi Bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.

Akifafanua, Waziri Mbarawa Amesema Makontena hayo 11,884 Yalikuwa na thamani ya Sh 47.4 Bilioni Wakati Magari Gari 2019 zenye Thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa Bandarini pasipo kulipiwa tozo.

Makontena Hayo Yalitolewa katika Bandari kavu ni MOFED 61, DICD 491, JEFAG 1, 450, AZAM 295, PMM  779, AMI 4384, TRH 4,424 Ambazo kodi yake ni Zaidi ya sh.Bilioni 47.
Magari 2019 Yalitolewa Bila kulipa kodi katika kampuni za  TALL 309, CHICASA 65, FARION 18, SILVER 97, MASS 171, HESU 1359 na kunyima nchi kodi yenye thamani zaidi ya Tsh.bilioni moja (1).

Waliotiwa Mbaroni na Jeshi la polisi Baada ya kukamatwa  leo ni John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally ,Masoud Seleman na Benadeta Sangawe.
Wanaotafutwa kwa Tuhuma za kusababisha Upotevu wa kodi za serikali katika Bandari ya Dar es Salaam ni Happygod Naftal, Nathan Edward, Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Benasweet Kamaina, Zainab Bwijo.

CUF Watoa Tamko Zito


Ismail Jussa Akizungumza na Waandishi wa Habari

Na Kalonga kasati

Kufuatia Taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Baada ya kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi, Tarehe 27 Desemba, 2015, Waandishi wengi Wa Habari Wametupigia simu wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi Taarifa ile.
Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida Yetu kutolea Taarifa Maamuzi ya Vikao vya Vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na Shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa Sababu Yale Yaliyokuwemo kwenye Taarifa hiyo yaligusia Pia Mazungumzo Yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata Ufumbuzi wa Mgogoro wa Uchaguzi Uliofanyika Tarehe 25 Oktoba, 2015.
Baada ya kuipitia Taarifa ya CCM na Mengine Yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Wa CCM Zanzibar wakati akitoa Ufafanuzi wa Yale yaliyomo kwenye Taarifa hiyo, CUF Tunapenda kuwaeleza Wazanzibari
Taarifa yenyewe Haionekani kama imeandaliwa na watu Makini wala Haioneshi kama walioitoa wanajua nini kilichopo. Hilo liko wazi kutokana na Taarifa yenyewe kuwa na Maudhui Yanayopingana ambayo Yamekuja kukorogwa Zaidi na maelezo Yaliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar Mbele ya Waandishi wa Habari na kuoneshwa katika Vituo kadhaa vya Televisheni: Taarifa inawataka Wanachama wa CCM Wajiandae na Uchaguzi wa Marudio lakini papo hapo inaeleza kwamba kikao kimeridhia Mazungumzo Yanayoendelea Ikulu Zanzibar. Taarifa haisemi iwapo Maamuzi ya vikao vya Mazungumzo hayatakuwa na Suala la kurudiwa Uchaguzi, Upi ni Mwelekeo wa CCM.
 Taarifa inazungumzia uchaguzi wa Marudio lakini papo Hapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anasema CCM Haina imani na Tume ya Uchaguzi iliyopo na kwa hivyo Uchaguzi huo wa marudio lazima Ufanyike chini ya Tume mpya. Baada ya hapo Hasemi Tume iliyopo ambayo muda wa Utumishi wa Makamishna wake unalindwa kikatiba itaondolewa vipi na Tume mpya itapatikana vipi.
Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini Katibu wa itikadi na Uenezi anasema hata Usiporudiwa ndani ya siku 90, Bado Dk. Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais.

Nukta hizi tatu ambazo haziwezi zote kusimama kwa pamoja bila ya kupingana Moja Dhidi ya nyingine zinaonesha tu ni kwa kiasi gani viongozi wa CCM Zanzibar Wamepoteza mwelekeo na hawana uhakika wa nini kitatokea katika kuondokana na Mgogoro huu wa kutengenezwa.
 Taarifa ya CCM haiwasaidii wanachama wa CCM wala wananchi wa Zanzibar kwa kuwapa matumaini ya kumalizika kwa mgogoro wa kutengenezwa wa uchaguzi wa Zanzibar na badala yake inaonekana imelenga kuwachanganya zaidi wananchi kwa maelezo yanayopingana.
Taarifa inaonyesha ni jinsi gani CCM kilivyopoteza mvuto kwa kujiweka mbali na wananchi. Taarifa hiyo inapongeza eti kuwepo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wakati wananchi wa Zanzibar, bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, siyo tu wanumia kutokana na sera mbovu za CCM lakini sasa wanazidi kuteketea na maisha yao kuwa magumu zaidi kutokana na fadhaa (tension) na taharuki iliyopo katika nchi kutokana na kutokuwepo kwa Serikali yenye ridhaa yao.

Harakati za maisha zimeathirika sana huku bidhaa vikiwemo vyakula vikipanda bei. Viongozi wa CCM hawaonekani kujali hali hii mradi wao yao yanawaendea. Tabia hii ya CCM kutowajali wananchi wanyonge wa nchi Hii ndiyo iliyopelekea wananchi kukiadhibu chama hicho katika uchaguzi mkuu na kupelekea mgombea wake wa Urais wa Zanzibar na wagombea Uwakilishi kushindwa vibaya kwa Tofauti ya zaidi ya kura 25,831. Taarifa inaendeleza utamaduni wa Unafiki wa kisiasa kwa eti kuwapongeza Viongozi wa CCM na jumuiya zake kwa kazi ya kukiimarisha chama chao huku wakijua kwamba viongozi wao hasa wale walioongoza Kamati ya Kitaifa ya Kampeni za CCM Zanzibar walishindwa kazi na kupoteza Mwelekeo.
Matokeo ya kazi mbovu ya Kamati ya Kampeni ya CCM Zanzibar ni kukisababishia Chama hicho kipigo kikubwa katika uchaguzi Huo kilichopelekea kushindwa katika nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa zaidi ya kura 25,831 na kupoteza viti tisa (9) vya Uwakilishi kisiwani Unguja mbali ya kutopata Hata kiti kimoja kisiwani Pemba. Viongozi hao Walishindwa kuwajibika licha ya Kutumia Mabilioni ya fedha walizopewa kwa ajili ya kampeni.
 Katika maelezo yake ya ufafanuzi kwa Waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar Anaitupia lawama Tume nzima ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kushindwa kazi Huku akijua na ikijulikana na kila Mmoja kwamba Tamko la kufuta uchaguzi limetolewa na Jecha Salim Jecha kinyume na Katiba, kinyume na Sheria ya Uchaguzi na kinyume na Maadili ya kazi yake.

Katiba inataka Jecha achukuliwe hatua za kufukuzwa kazi kwa kuanza na kumuundia Tume Maalum ya kumchunguza, na siyo kutafuta mbinu za kumlinda kwa kuwaingiza Wasiokuwemo.
Maelezo ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar kwamba Dk. Ali Mohamed Shein Ataendelea kuwa Rais Hata Baada ya Miezi Mitatu ni kielelezo na Ushahidi Mwengine wa Jinsi CCM isivyoheshimu Katiba.

Kwa hakika, hili suala la kutaja siku 90 Ambalo linatajwa sana na CCM na wapambe Wake haijulikani hata linatokea wapi. Hakuna Pahala popote katika Katiba ya Zanzibar wala Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar panapotajwa Sharti la kurudiwa Uchaguzi ndani ya siku 90 kwa sababu Katiba yenyewe na Sheria ya Uchaguzi Haina sehemu yoyote inayozungumzia kufuta Uchaguzi na kufanya Uchaguzi wa Marudio.
 Kwa Ujumla, Taarifa ya CCM Zanzibar iliyotolewa na Katibu Wake wa itikadi na Uenezi inaonyesha jinsi chama hicho kisivyojali Madhila Wanayoyapata Raia, Fedheha iliyopata Taifa na Hali ya kiuchumi inayozidi kudorora kila siku Zanzibar ikiwaathiri Mno Wananchi wanyonge.
Baada ya Uchambuzi huo wa Taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, CUF inapenda kuwaeleza Wazanzibari Waipuuze Taarifa hiyo ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar kwani Haina lolote Jipya Zaidi ya kutaka kufunika kombe kutokana na Hali Ngumu inayotokana Na Hoja za viongozi wa Ngazi za chini na Wanachama wa CCM Wanaotaka Maelezo ya kwa nini Chama hicho licha ya kutumia Mabilioni ya shilingi kimeshindwa vibaya katika uchaguzi mkuu.


Wazanzibari wasubiri taarifa rasmi ya matokeo ya mazungumzo yanayowahusisha viongozi wakuu wa kisiasa yanayofanyika Ikulu Zanzibar ambayo yamo katika hatua za mwisho kumalizika.
 Wampe nafasi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli, Ambaye Anaendelea na Juhudi katika Ngazi za Juu kabisa za kuhimiza kupatikana Ufumbuzi wa Haraka wa Mgogoro Wa Uchaguzi wa Tarehe 25 Oktoba, 2015.
 CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba Haitotetereka na itasimamia kwa dhati Maamuzi yao waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia Uchaguzi Mkuu wa Tarehe 25 Oktoba, 2015 na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao.

 inaendelea kuwapongeza Wazanzibari kwa kuonesha Ukomavu wa Hali ya Juu wa kisiasa Na kuendelea kutunza Amani na Utulivu Wakati Wakisubiri Matokeo ya kazi kubwa Waliyoifanya Tarehe 25 Oktoba, 2015 Ambayo inaashiria Ujenzi wa Zanzibar Mpya.

Sunday, 27 December 2015

Waliosafiri Nje ya Nchi pasipo kibali Hatma Yao ipo kwa Rais

 
 
 Rais Dkt John Pombe Magufuli
 
 Na Kalonga Kasati

Adhabu inawanyemelea watumishi wa serikali Waliokaidi Agizo la kutosafiri nje ya nchi bila kibali cha Rais John Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Habari Zilizopatikana kutoka Baadhi ya Wizara  zilieleza  kuwa Tayari Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara Wameshapewa Orodha ya Majina ya Watumishi Waliosafiri Nje Ya nchi kinyemela.

Chanzo kimoja cha habari kimesema  kuwa tayari majina hayo yamepatikana na kinachofanyika sasa ni kupitia taratibu, sheria na kanuni kabla ya kuwachukulia hatua.

Watumishi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wamesimamishwa kazi kwa kwenda nje ya nchi licha ya maombi yao ya kusafiri kukataliwa na mamlaka.

Jana   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Donald Mmbando  alikiri kukabidhiwa taarifa kuhusu Watumishi waliosafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu na kwamba kwa sasa kuna Taratibu ambazo zinafanyiwa kazi na ngazi Husika kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.

Ni kweli niliagiza Nipatiwe Taarifa ya Watumishi Hao na Nimeshapewa ila kuna Taratibu Ambazo zinafanyiwa kazi na zitakapokamilika itatolewa Taarifa ya wale wote Waliosafiri na Wamefanywa nini,” Alisema Dk. Mmbando.

“Kwa Sasa Siwezi kulizungumzia ila likikamilika Tutawajulisha.” Hivi karibuni Dk. Mmbando Alitoa Taarifa kwa Wakuu wa Idara wizarani kwake Akiwataka ifikapo Desemba 21 Awe Amepata Taarifa ya Wale Wote Waliokiuka Agizo la Rais la kutosafiri nje ya Nchi.

Dk. Mmbando Aliandika Dokezo kwenda kwa Wakuu wa idara hiyo Ambayo iliwataka kuwataja Watumishi Walio chini yao Ambao Walisafiri nje ya nchi Baada ya katazo la Rais Dk. Magufuli.

Katika Dokezo hilo Walitakiwa kueleza Watumishi hao wamesafiri kuelekea nchi gani, Tarehe ya safari, madhumuni ya safari hizo, Safari hizo zimegharamiwa na nani pamoja na kiasi cha fedha kilichotumika.

Waliosimamishwa kazi Takukuru ni Msemaji Doreen Kapwani, Mary Mosha, Ekwabi Mujungu na Rukia Nikitas. 

Awali, Ofisi ya Rais ilisambaza mwongozo kwa Taasisi na Mashirika ya Umma Unaoweka Masharti ya ambayo Watumishi wa umma Wanaotaka kusafiri Nje ya nchi Watatakiwa kuyatimiza ili Wapewe kibali cha kusafiri.

Masharti hayo ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi Sefue na Maombi Hayo Yawasilishwe kwa Msajili wa Hazina kabla ya kwenda kwa Sefue ili Mwombaji Aweze kujenga Hoja kwa kuzingatia Umuhimu wa Safari hiyo na Tija itakayopatikana kutokana Na Safari hiyo.

Masharti hayo Yanamtaka Mtendaji Mkuu wa Shirika ama Taasisi Apime Aonekane kama Safari Hiyo ni Muhimu  kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi kabla ya kuwasilishwa Hazina.

Sharti lingine ni Umuhimu wa safari hiyo na isipofanyika itaathiri vipi Taifa na Mwombaji  Aeleze Manufaa ya Safari hiyo kwa taasisi na Taifa kama imewahi kufanyika Huko Nyuma.

Ofisi za Umma zilipokea barua kutoka kwa Msajili wa Hazina Novemba 12 Mwaka huu ikieleza kuwa Rais Magufuli Ametoa zuio la Jumla kwa Safari za nje ya nchi katika Utumishi Wote wa Umma na Mihimili yake. Barua Hiyo ya Hazina ilisema zuio hilo litadumu Hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kimesema Mchakato Wa Kumpata katibu Mkuu Wake Utaanza Mwakani




Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Aikaeli Mbowe
 
Na Kalonga Kasati

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema mchakato wa kumpata katibu Mkuu Wake Utaanza Mwezi ujao.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Mwenyekiti wa Chama Hicho, Freeman Mbowe kwa Mujibu Wa Katiba ya chama Hicho, Ndiye Mwenye Jukumu la kupendekeza Jina la Katibu Mkuu Na kulipeleka katika Baraza Kuu kupigiwa kura, kisha kupitishwa.

Tangu Agosti 3, Katibu Mkuu wa Chama Hicho Dk Willibrod Slaa Alipumzishwa na Baraza Kuu Baada ya kutofautiana na Kamati Kuu Baada ya Chama Hicho kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu Ndiyo Anakaimu Nafasi iliyoachwa Wazi na Dk Slaa.

Mchakato wa kumpata Katibu Mkuu umeanza kuibua hali ya Sintofahamu, Huku Majina Mbalimbali ya Vigogo wa Chama Hicho Yakitajwa, likiwemo la Waziri Mkuu wa Zamani, Frederick Sumaye Ambaye hivi karibuni Alitangaza Rasmi kujiunga na Chadema.

Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema Ibara ya .6.3.5. inasema; (b) Nafasi wazi za Uongozi Walioteuliwa Zitazibwa na Vikao Husika kwa kufanya Uteuzi Mpya katika Muda Usiozidi Miezi Mitatu Tangu Nafasi kuwa Wazi, (c) Muda wa Uongozi wa Muda kwa Mujibu wa kifungu 6.3.5 (b) Hautazidi Mwaka Mmoja (d) Bila kujali sharti la kifungu 6.3.5 (c) Hakutafanyika uchaguzi Rasmi wa kuziba Nafasi kama kumebakia miezi sita tu au chini Ya Hapo kabla ya Uchaguzi mkuu wa kawaida Wa Chama Unaofuata kufanyika.

Akizungumzia Mchakato huo, Mwalimu Alisema Baraza Kuu litakutana mapema Januari mwakani, kujadili masuala mbalimbali, likiwamo la kumpata Katibu Mkuu.

“Si kama chama kimekaa muda mrefu bila Katibu Mkuu. Yupo anayekaimu na kinachofanyika sasa ni kumpata Katibu kamili.”

Baraza Kuu lilikutana litajadili Suala hilo kwa kina na kuja na Mapendekezo Mbalimbali,” Alisema Mwalimu na kusisitiza kuwa kila Jambo litafanyika kwa Mujibu wa Katiba ya chama hicho.

Alisema Uongozi wa Muda Ndani ya Chama Hicho Hauwezi kuzidi Mwaka Mmoja na Nafasi ya kuteuliwa Muda wa kukaa wazi Hauzidi Miezi Mitatu kabla ya kuteuliwa kiongozi Mwingine.

Dr Amtaka Gwajima Awaombe Radhi Maaskofu na Watanzania



Dr Wilbroad Peter Slaa
Na Kalonga Kasati
Baada ya Askofu Gwajima kusema kuwa Hakuwa Akimuunga mkono Lowassa, Dkt. Slaa amemtaka Awaombe Radhi Maaskofu Pamoja na Watanzania kwa kuwadanganya. 
 
Amesema Hakutegemea Askofu Gwajima kumkana Hadharani Lowassa

  Ni muhimu kwa Mshenga Gwajima kutubu na kuwaomba Radhi Watanzania kuliko kuendelea kuwapotosha.
 
 Mungu hamilikiwi na binadamu awaye yote. Watanzania tunawajibu wa kumshukuru sana Mungu kwa kutukomboa na kutuokoa na "Mabadiliko ya  Kuzungusha Mikono Mshenga Na Ukawa yake walitaka kutuaminisha sote kuwa Mabadiliko ni kuzungusha mikono! Walitaka kutuaminisha kuwa "Mabadiliko ni Lowassa na Lowassa ni Mabadiliko

Lowassa Aligeuzwa kuwa Ajenda Badala ya Ajenda za Msingi za Wananchi. Mungu Amesikiliza Sala za Wanyonge na Walalahoi. Namshukuru Sana Mungu aliyenionyesha kuwa kati ya Wawili hao, Japo Wote kila mmoja Ana Uchafu, Magufuli ni "Nafuu mara eflu" kuliko fisadi Lowassa. Asante sana Mungu Mwema kwa kulinusuru Taifa lako lililotaka kuingizwa Mjini na Makuwadi kwa Ulaghai na Upotoshwaji Uliopitiliza.

  Nilimtaka Gwajima Awaombe Radhi Maaskofu Aliosema Wamehongwa na Lowassa na kuwa fedha Hizo Waligawiwa Mbele ya Maovu Yake.
 
 Alisema Bila kumumunya Maneno, kuwa Maaskofu wa kilutheri Alikwisha Malizana nao" Na kuwa kati ya "Maaskofu wa Kikatoliki 34 Wamehongwa Maaskofu 30 na kumtaja kwa Jina Askofu Mkuu Mmoja, ambaye yeye kapewa fedha za kununulia Gari la kiaskofu." 
 
Fedha Hizo Alidai Zimetolewa na Lowassa kupitia Rostam Azizi. Gwajima, Tambua kuwa kama ni kweli Toka tena Hadharani wakemee Maaskofu wanaopokea Rushwa, na kama si kweli Waombe Radhi Hadharani Maaskofu Hao kwani kauli Hiyo ilitaka kuwagawa Maakofu na kuwachafua.

Lakini, alitamka Hayo Akiona ni Sifa, ndiyo Maana Nilimshangaa Kiongozi wa Dini Ambaye Badala ya kukemea Anaona ni sifa. Kama Wenzangu Waliokuwepo na Wao wana Misingi ya kusimamia Basi Watatoa Ukweli Wao, na kama wanachukia ufisadi basi Watatoka Hadharani kukemea tamko hilo lililotolewa Mbele yetu Watu 4 Akiwemo Mshenga.

Nilipotamka Hivi Wengi Walidhani Dr. Slaa ndiye Katamka kuwa Maaskofu Wamehongwa. Kama Askofu Anaweza kufika Mahali Akawasingizia Wenzake ni Hatari Sana na Halihitaji kufungiwa Macho na Masikio. 
 
Kama Anavyosema Gwajima ni " kweli". Basi Wote Tunaopenda kupiga vita Ufisadi ni lazima tupaze sauti zetu, na kukemea kitendo hicho kama kweli kimefanywa na wale tunaotegemea kusimamia Maadili katika Jamii Yetu.
 
Wako Walioniambia Dr. Slaa unapata wapi Ujasiri wa kuwasema Viongozi wa Dini. Sijawahi kuyumba wala kuyumbishwa. Ukweli Utatamkwa hata kama ni Mchungu, na Uovu Na uozo utasemwa tu Hata kama Umetendwa Na nani. Ukitazama Nyuso za Wazi  haki Haitatendeka Milele.

  Katika Busara ya kawaida, Hatukutegemea Gwajima kujitokeza "Kumkana Lowassa" hasa kabla ya kuomba Radhi. Aidha Kauli " Live" kwenye YouTube na Mitandao Mbalimbali ziko Bado kibao. Ama kweli Gwajima ni kiongozi asiye na Dhamira kukanusha kauli zake hizo kabla ya kuomba Radhi.

Wako watakaodhani kuwa Dr Slaa ana Bifu Binafsi na Gwajima. Ni kweli kibinadamu Nimeumia Sana kwa kuwa kuumizwa na rafiki kunaumiza sana, lakini nawaonea huruma zaidi Watanzania Waliobebwa kwa ushabiki Mkubwa na kupoteza Nguvu zao nyingi na labda "kupoteza Fursa ya kuiondoa CCM kwa Muda mrefu Ujao" kwa kuwaamini watu kama kina Gwajima. Hiki ndicho kinachonisukuma Zaidi kuendelea kumkaba Gwajima Hadi Atakapoomba Radhi kwa watanzania wanyofu.

Nawaomba Watanzania Tuwe na kumbukumbu. Tuzisikilize Tena Kauli Mbalimbali Alizozitoa Gwajima, Tena Wakati Mwingine kwa Njia ya Maombi kwa Jina la Mungu. Hali Hii isipokemewa kwa Ukali Sana Ni Hatari sana.

Wachimbaji Wadogo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Kuandamana


Wachimbaji wadogo wa Tanzanite wapinga kufungiwa migodi yao


8c6650e7-7156-45ae-b006-02e64a1bc497Mwanachama wa Chama cha Wachimbaji Wadogo Wa Madini ya Tanzanite (Marema) Tawi la Mji Mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Omary Mandari Akizungumza kwenye Mkutano Wao Ambapo Waliazimia kuandamana kwa Amani kupinga Migodi yao 19 kusimamishwa kufanya kazi.38941dfc-84bd-4129-bf67-bb25162cfbdeMwanachama Wa chama cha Wachimbaji Wadogo Wa Madini ya Tanzanite (Marema) Tawi la Mji Mdogo Wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Zephania Joseph Akizungumza kwenye Mkutano Wao Ambapo Waliazimia kuandamana kwa Amani.

Saturday, 26 December 2015

Gwajima Amekataa Kuwa Hakuwahi Kumuunga Mkono Lowassa


Image result for askofu gwajima
Mchungaji Josephat Gwajima wa Ufunuo

Na Kalonga Kasati

Mchungaji Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima Amejitokeza Hadharani  na kukana kwamba Hakuwahi kumuunga Mkono Edward Lowassa Wakati Wa kampeni za Urais.

Akiongea katika Mahojiano Maalumu na kituo Cha Azam Tv, Gwajima Amesema yeye Hakuwahi kuwa Mshirika wa Lowassa wala Chama chochote, Bali Aliitwa Jijini Arusha na Jangwan Dar es Salaam  kwa Ajili ya Maombi Tu na SiVinginevyo

Amesema kitendo cha kukubali Wito huo wa Maombi kimewafanya Watanzania Walihisi kwamba Yeye alikuwa Team Lowassa, kitu Ambacho sio kweli.

Amedai yeye alikuwa Mfuasi wa Mabadiliko ya nchi, Alikuwa Akiunga Mabadiliko ya nchi Na Sio Personality ya Mtu au chama cha Mtu.

Wakati Gwajima Akikana kumuunga mkono Lowasaa, kumbukumbu Zinaonyesha kuwa Mchungaji Huyo Alikuwa ni Team Lowassa na  Alikuwa Mstari wa Mbele kuhakikisha Mheshimiwa Lowassa Anashinda kiti cha Urais.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Gwajima Alitumia Nguvu kubwa Sana Wakati wa kampeni kupambana na Dr Slaa ambaye Wakati huo Alikuwa Akishusha Makombora Mazito kuhakikisha Lowassa Hashindi huku Akimtuhumu Gwajima kuwa Mshenga wa Lowassa Aliyemfuata kumpigia debe Wampokee Chadem
a