Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema nchi
haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania utosikiliza kampeni
za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya
chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la kupandisha
bei za vyakula.
Amesema Serikali ndio yenye jukumu la
kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa
zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na
Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya
kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo
kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa
watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.
“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya
chakula cha zaidi ya tani milioni tatu hali iliyopelekea baadhi ya
Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi,
ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa
akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.
Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na
Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki
zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili
kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.
“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa
sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo
amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi
yanayostahimili ukame.
Waziri Mkuu amesema kwamba endapo
kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya
upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Kuhusu kupanda wa bei ya
vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa
chakula katika nchi jirani.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
- L. P. 980,
DODOMA.
JUMATATU, JANUARI 16, 2017.
No comments:
Post a Comment