Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan akitoa ufafanuzi kuhusu uwekaji
wa kituturi cha kupigia kura wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa
Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata
watakaosimamia uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20
za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Januari 22, 2017 leo
mjini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo ya Wasimamizi
wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata
kutoka Kanda ya Kaskazini na Pwani wakiendelea na mafunzo ya kuwajengea
uwezo wasimamizi hao wakati uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika
katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani
Januari 22, 2017.
Kaimu Naibu –Uendeshaji wa
Uchaguzi, Bi. Irene Kadushi Tutah akiwasilisha mada kuhusu Kujumlisha
na Kutangaza Matokeo ya Ubunge na Madiwani wakati wa mafunzo ya
Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo
na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22, 2017.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan akionyesha mfano wa namna ya
kuweka vituturi vya kupigia kura vituoni ili kuwawezesha wananchi kupiga
kura kwa wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Madiwani
utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la
Dimani Januari 22, 2017.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo
wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri wakifuatilia kwa makini mafunzo ya
Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo
na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo Januari 22, 2017 mjini Dodoma.
Picha na Aron Msigwa – NEC
No comments:
Post a Comment