Kiungo wa Leicester city Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka.
Mahrez mwenye miaka 25 raia wa
Algeria aliyeisaidia Leicester kushinda taji la ligi kuu soka England
msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mcehzaji bora wa England
sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika.
Mshambuliaji wa Senegal na klabu
ya Liverpool Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya
taifa ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang walikuwa wakiwania tuzo hiyo
pia.
Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
Denis Onyango wa uganda na klabu
ya Memelodi Sundowns akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi
za ndani ambayo mwaka jana ilichukuliwa na Mtanzania Mbwan Samatta hivyo
imerudi tena ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Mchezaji bora kwa kina dada
imeenda kwa Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku
timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda.
No comments:
Post a Comment