Thursday, 13 July 2017

Trump na Putin waondoa tofauti zao

Putin na Trump walikutana mjini Hamburg
Rais wa Marekani Donald Trump anasema anaelewana vyema na rais wa Urusi Vladimir Putin.
Alihojiwa na kituo cha Christian Broadcasting Network, siku chache baada ya mkutano uliokuwa ukisubiriwa kati yake na Putin wakati wa mkutano wa G20 mjini Hamburg.
Trump pia amesema kuwa alikuwa na uhakika kuwa Putin angependa Hillary Clinton akiwa madarakani
Uchunguzi unaendelea kufuatia madai kuwa Urusi ilimsaidia Trump kuchaguliwa.
Trump anakana kufahamu hilo na Urusi nayo mara kwa mara imekana kuingilia kati.
"Sisi ni nguvu kubwa ya kinuklia, sawa na Urusi. haitoi maana yoyote ikiwa tutakosa kuwa na uhusiano."
Uchunguzi unaendelea kufuatia madai kuwa Urusi ilimsaidia Trump kuchaguliwa.
Bwana Trump alitaja usitishwaji wa hivi majuzi wa mapigano kusini magharibi mwa Syria kama njia moja ya kuonyesha ushirikiano na Bwana Putin.
Trump pia alitumia mahojiano hayo kukana madai kuwa Urusi ilichangia kuchaguliwa kwake.
Mapema Trump alimtetee mwanawe Donald Trump Jr, kuhusu mkutano aliofanya na wakili wa Urusi mwaka 2016 wakati wa kampeni ya urais nchini Marekani.

Mwana wa Trump alikutana na wakili Natalia Veselnitskaya katika jumba la Trump Tower mweze Juni mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment