Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa
mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa
wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza
majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo na
kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya sheria na
taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye lengo
la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto
wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, akizungumza na kikosi cha Polisi wanawake baada ya
kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili
mkoani Singida, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na
kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza
majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Na Jeshi la Polisi Nchini
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa
pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji wa Jeshi
hilo hatua ambayo italiwezesha ieshi hilo kufanyakazi zake kwa weledi
katika kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.
IGP Sirro, amefanya ziara hiyo
ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi
hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa ili
kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.
Katika mazungumzo yake IGP Sirro,
amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki na
bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha
upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.
Hata hivyo, katika mabaraza ya
kuzungumza na askari na maofisa baadhi ya hoja kadhaa ziliibuliwa kwa
baadhi ya askari waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao, ambapo IGP Sirro
aliahidi kuzishughulikia mapema ili kuzidisha morari katika utekelezaji
wa majukumu yao ya kila siku.
Aidha, katika ziara yake IGP
Sirro, alipata fursa ya kukutanana Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na
Usalama ya mkoa huku masuala kadhaa ya kiusalama na mbinu na mikakati
ikijadiliwa katika kamati hizo na kuahidi kutoa ushirikiano
utakaowezesha kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu.
No comments:
Post a Comment