Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka kwa wananchi.
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara Bw. Gambo amesema ni vyema
migogoro hiyo inapojitokeza ikatatulia kwa njia ya mashauriano kwa pande
zinazo kinzana badala ya wananchi kujichukulia sheria mikononi ya
kuvamia mashamba hayo.
"Ni kosa kwa wananchi kuvamia mashamba ambayo yana hati miliki halali,
serikali ya haitavumilia kuona vitendo hivyo vikiendelea tutachukua
hatua kwa wale wote watakaobainika kufanya uvamizi huo", amesema Gambo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmshauri ya Meru, Christpher Kazeri
amesema wamekua wakiifanyia kazi migogoro hiyo huku afisa mipango miji
wa Halmashauri hiyo Shahidi Chuma, ameahidi kutafuta suluhu ya migogoro
hiyo baina ya kijiji cha Magadini na maloloni.
No comments:
Post a Comment