Tuesday, 25 July 2017

Justine Bieber afuta matamasha yake bila kutoa sababu


Mwanamuziki wa mtindo wa Pop Justine Bieber amefutilia mbali safari yake ya kikazi katika miji iliyo tajwa kufanyka mjini Los angeles nchini Marekani bila kutoa sababau yoyote ya kufikia maamuzi hayo
Tamasha lilofutwa lita athiri ratiba ya matamasha ambayo yangefanyika terehe 14 Amerika ya kaskazini na tarehe 10 mwezi oktoba barani Asia na ianelezwa wazi kwamba sasa gharama za kiingilio zitarejeshwa kwa mashabiki wake.
Taarifa iliyo tolewa na uongozi wa masanii huyo ina sema Bieber anawapenda mashabiki wake na hapendi kuwakwaza na akatumia fursa hiyo kutoa shukuruni zake kutokana na uhusiano mzuri ambao umekuwapo baina yake, uongozi na wasaidizi wake kwenye matamasha zaidi ya 150 katika mabara 6 tofauti.
Hatua hii inakuja baada ya kutafakari kwa kina msanii huyo nyota wa pop ameamua hataimba tena kwenye matamasha yaliyo salia ,Bieber mwenye miaka 23 hajatoa kauli yoyote wala kuandika chochote kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii
Mtandao wa celebrity news ulikinukuu chanzo kimoja na kuarifu kuwa mwanamuziki huyo raia wa Canada amefutilia mbali matamasha yaliyo salia sababu bila za msingi
Mwishoni mwa juma msanii huyo alipigwa picha akitembea mlimani na mjini Los angeles akiwa na na binti mdogo ambaye walionekana kuwa na mahusiano mazuri
Justine Bieber alianza mkururu huu wa matamasha kwa nguvu kubwa ya albamu yake ya "purpose" aliyoitoa mwezi march mwaka 2016 na tayari ametumbuza matamasha zaidi ya 150 kwenye bara la Ulaya, Afrika, Amerika ya Kusini, Australia na maeneo ya bara Asia
Hatua hii ya Bieber inakuja siku kadhaa baada ya msanii huyo kukatazwa kufanya matamasha nchini China sababu ya tabia mbaya kama ilivyo arifiwa na mamlaka mjini Beijing

Licha ya kusifia mapenzi waliyo nayo mashabiki kwa msanii huyo lakini mamlaka hizo haziku weka wazi ni tabia zipi za kukera alizo zionyesha msanii huyo kiasi cha kukatazwa kufanya matamasha nchini humo

Bieber toka alipoanza muziki amekuwa kama mwizi wa mioyo ya mashabiki wake kwa mapenzi makubwa waliyo nayo kwake na kazi zake.

No comments:

Post a Comment