Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema maombi ya kujiunga na elimu ya
juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yatatumwa moja kwa moja vyuoni.
Akizungumza leo Julai 20, Kaimu Katibu Mtendaji TCU, Profesa Eleuther
Mwageni amesema hawatapokea maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kama
ilivyokuwa hapo mwanzo.
Maombi ya kujiunga na elimu ya juu yataanza kupokelewa rasmi Julai 22 kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu nchini.
"Wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu wasisite kuchagua vyuo
wanavyovipenda na kuhakikisha wanakuwa makini na programu zilizowekwa na
vyuo iwapo zinatambuliwa na Tume," Amesema.
Amesema TCU haitatoza ada yoyote ya udahili kwa waombaji.
No comments:
Post a Comment