Madaktari bingwa kutoka China wakifuatilia ufunguzi huo
Daktari Bingwa kutoka China
akipokea mkono wa asante kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla
mara baada ya kupokea Cheti cha shukrani alichokabidhiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri
Dk.Kigwangalla akimuongoza Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggrey
Mwanri amezindua rasmi kambi maalum ya huduma za Afya juu ya upimaji wa
Afya bure kwa wananchi mbalimbali Wilayani Nzega, ndani ya Hospitali ya
Wilaya ya Nzega.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanri ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwapongeza
waandaaji wa kambi hiyo kwani itasaidia kuboresha afya za wananchi ili
kuwa na afya njema.
“Wananchi wanahitaji Afya njema,
tunapongeza kwa kambi hii kwani madaktari bingwa waliokuja hapa watatua
matatizo ya msingi kwenye afya zetu. Hivyo wananchi mujitokeze kwa
wingi” aleleza RC Mwanri.
Aidha, Mh. Mwanri amewapongeza
Madaktari bingwa kutoka China ambao wanaendesha kambi hiyo ya siku
Sita, iliyoanza rasmi Julai 24 na inatarajia kumalizika Julai 30.
Hata hivyo, Mh. Mwanri aliwaagiza
Wakurugenzi wote wa Mkoa wa Tabora waupokee mpango huo wa kambi za
huduma za Afya ili uende mkoa mzima kwani wanakosa fursa ya kuonana na
Madaktari bingwa.
“Ni jambo zuri, tunaomba
Wakurugenzi wote mulipokee suala ili wa Mkoa wa Tabora ili liendelee
Mkoa mzima. Pia ni wasaha kwa wananchi wote kupeana taarifa ili zienee
kwa watu wote wajitokeze hapa Nzega kupatiwa huduma za upimaji na
matibabu.” Alieleza Mh. Mwanri huku akimuagiza Mganga Mkuu ahakikishe
anaratibu mpango huo uenee Mkoa nzima wa Tabora.
Kwa upande wake,Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi
Kigwangalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini ameshukuru Serikali
ya China kwa kufanikisha tukio hilo ikiwemo kutoa dawa za Maralia kwani
kwa msingi huo utasaidia kuokoa maisha ya wananchi wa Nzega.
“Tunapokea kwa mikono miwili
msaada huu wa kutoka Serikali ya China hasa kupitia kwa Balozi wake hapa
nchini Tanzania. Dawa hizi ni nyingi nahakika zitasaidia wananchi wote
kuanzia wilaya ya Nzega na Mkoa nzima wa Tabora kwa ujumla. Nawashukuru
sana wananchi wanaojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuja kupata huduma
za matibabu kwenye kambi hii ya madaktari bingwa hapa Nzega” alieleza
Dak. Kigwangalla.
Zoezi hilo la Upimajj wa Afya Bure
Wilayani Nzega, limeandaliwa na Wabunge wa majimbo yote ya Nzega
ambapo imeanza kuanzia hiyo Julai 24 na itatarajiakumalizika Julai 30,
huku kwa wakazi wote wa Nzega na jirani wata pima afya zao bure na
kupata huduma za matibabu bure, ikiwemo upasuaji.
Tayari timu ya Madaktari bingwa wa kila fani ya tiba wapo kwenye kambi hiyo inayoendelea kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nzega.
No comments:
Post a Comment