Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanyara wilayani Mbozi ambao
walikusanyika barabarani wakitaka asimame na kuzungumza nao . Alikuwa
akitoka Vwawa kwenda Uwanja wa Ndege wa Songwe Julai 24, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary (kushoto kwake) wakiagana na viongozi wa Mkoa wa Songwe kabla
ya kuondoka kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa huo kwenda kwenye uwanja wa
ndege wa Songwae baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani humo Julai 24,
2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea silaha za jadi kutoka kwa Chifu Muleshwelwa Mzunda wa Mbozi
ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chief wa Songwe Julai 24, 2017.
Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe . Kushoto
kwake ni mkewe Mary na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku
Galawa.
Baadhi ya watumishi wa umma,
viongozi wa dini na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipozungumza nao katika kikao cha majumuisho kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Sunrise wilayani Mbozi Julai 24,
2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi
katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya
Sekondari ya Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. Kulia ni mkewe
Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa na wapili kulia ni
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Songwe, Erasto Zambi.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment