Jeff Bezos.
Mwanzilishi wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos amempita Bill Gates na kuwa
tajiri namba moja duniani akimiliki utaji wa dola za kimarekani 90.6
bilioni (Tsh 203 trilioni).Kupanda wa hisa za Amazon kwa asilimia 1.5 jana Alhamisi Julai 27, kulimaanisha kuwa tajiri huyo amempita mwanzilishi mwenza wa Microsoft, kwa mujibu wa taarifa za jarida la Forbes la nchini Marekani.
Bill Gates.
Forbes wameeleza kuwa Bezos ana utajiri wa $90.6 bilioni akimzidi Bill
Gates aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo akiwa na utajiri wa $90 billioni
sawa na Tsh 201.5 trilioni.Bezos ananakadiriwa kumilikia hisa milioni 80 za Amazon akiwa ni mwenye hisa nyingi zaidi ya mwingine yeyote.
Kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa akijikita zaidi katika mradi wake wa Blue Origin unaohusika na urushaji wa rocket kwenda angani pamoja na Washington Post ambazo zote anazimiliki.
Warren Buffett.
Bezos ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu (CEO) wa Amazon
alizaliwa mwaka 1964 Albuquerque Jimbo la New Mexico na alisoma Sayansi
ya Kompyuta na Uhandisi wa Umeme katika Chuo Kikuu cha Princeton.
Mack Zuckerberg
Alipohitimu alikwenda kufanya kazi na Wall Street lakini mwaka 1994
aliacha kazi na kwenda kuanzisha Amazon ambapo kwa mara ya kwanza Amazon
ilianzishiwa katika karakana ya kutengenezea magari. Baada ya kampuni
hiyo kuanza kufanikiwa na kujipanua katika nchi mbalimbali, mwaka 2000
alianzisha kampuni ya Blue Origin inayojishughulisha na masuala ya anga.
Michael Bloomberg.
Mwaka 2013 akiendelea kujipanua, aliinunua Kampuni ya Washington Post
kwa $250 milioni na ilipofika Mei 2017 alitajwa kuwa na utajiri wa $
84.8 bilioni, lakini leo Julai 27, 2017 amefikisha utajiri wa $90.6
bilioni na kushikilia usukani wa mtu tajiri zaidi duniani.Kwa mujibu wa Forbes, hawa ndio matajiri 10 wanaoongoza duniani;
Jeff Bezos (53)- Amazon.com
Bill Gates (61)- Microsoft
Amancio Ortega (81)- Zara
Warren Buffett (86)- Berkshire Hathaway
Mack Zuckerberg (33)- Facebook
Carlos Helu (77)- telecom
Larry Ellison (72)- software
Michael Bloomberg (75)- Bloomberg LP
Bernard Arnault (68)- LVMH
Charles Koch (81)- diversified
No comments:
Post a Comment