Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiongea
na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Radio ya Efm Bw. Francis Ciza wakati
wa ziara yake kutembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na
watumishi wa Radio ya Efm (hawapo katika picha) alipofanya ziara ya
kutembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Radio ya Efm
wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo katika picha) alipotembelea chombo
hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na watendaji wa Radio ya Efm pamoja na watendaji
wa Wizara ya Habari wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea
na Viongozi wa Radio One na ITV alipofanya ziara yake IPP Media leo
Jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Radio One na
ITV Bi. Joyce Mhaville.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akipata
maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa ITV/Capital Tv Bw. Koigi Wacharia
wakati wa ziara yake kutembelea Chombo hicho cha Habari leo Jijini Dar
es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa) pamoja
na watendaji wa Wizara ya Habari wakiangalia namna mfumo wa urushwaji wa
habari unavyofanya kazi katika studio za ITV wakati wa ziara yake leo
Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa kushoto )
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Radio One/ITV na
watendaji wa Wizara ya Habari wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es
Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – MAELEZO
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali imeeleza kuwa inathamini
na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Vyombo vya Habari nchini katika
kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi na kwa wakati.
Akizungumza katika ziari yake
alipotembelea vyombo vya habari vya Radio EFM na Radio One/ ITV leo
Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa lengo kubwa la Serikali
ni kuwepo kwa ushirikiano mzuri na sekta ya habari nchini.
“Lengo la ziara hii ni kuimarisha
uhusiano baina ya Serikali na vyombo vya habari pamoja na kufahamu
utendaji wenu wa kazi na namna mnavyosimamia maudhui ya vipindi vyenu
mnavyoviandaa” amesema Prof. Gabriel
Aidha aliongeza kuwa ni jambo jema
linalofanywa na watanzania wazawa kuwekeza katika sekta ya habari kwa
kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na utandawazi kupitia taarifa mbalimbali
zinazotolewa zenye lengo la kuhabarisha na kujenga taifa letu.
Kwa upande mwingine Prof. Gabriel
amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kufanya kazi kwa
kuzingatia maadili, weledi na uzalendo ili kufikia malengo
waliyojiwekea.
Pia amewataka watumishi wa vyombo
hivyo vya habari kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa kujituma ili
kupata matokeo chanya katika soko la ushindani na kuifikia jamii kubwa
zaidi katika kutoa habari za uhakikia na zenye usahihi.
Sambamba na hilo Prof. Gabriel
amevitaka vyombo hivyo vya habari kuzingatia maudhui yanayoendana na
jamii ya kitanzania pale wanapoandaa vipindi mbalimbali ili kujenga
jamii yenye utamaduni mzuri ikiwemo kufanya kazi kimkakati.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Redio Efm, Bw. Denis Ssebo amesema kuwa uongozi wa radio yake upo
tayari kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali lengo likiwa ni
kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za utangazaji ili kufanya kazi
kwa kiwango chenye ubora .
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Radio One/ITV Bibi. Joyce Mhaville ameishukuru serikali
kupitia wizara ya Habari kwa kuonyesha ushirikiano mzuri na vyombo vya
habari ikiwemo kufanya kazi kwa karibu na kuviwezesha vyombo hivyo
kupata habari zenye ukweli na uhakika.
No comments:
Post a Comment