Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa
Kagera, Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP) Augusine Ollomi,
muda mfupi alipowasili, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi
yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua
chamgamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na
Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.
Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka askari wa Jeshi
hilo kufanyakazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na taratibu
zitakazosaidia kujenga taswira chanya hasa wanapotekeleza majukumu yao
ya kila siku.
IGP
Sirro, ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na askari na maofisa wa
mkoa wa Kagera, wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara zake zenye
lengo la kujitambulisha pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo
wakati wakitekeleza majukumu yao.
Alisema
kuwa, kila askari analojukumu mbele yake la kuhakikisha suala la
uhalifu na wahalifu linadhibitiwa hususan kwa kuimarisha usalama wa raia
na mali zao huku wakizingatia kuwa, mkoa huo unapakana na nchi jirani
za Uganda, Rwanda na Burundi.
Hata
hivyo, katika ziara yake, IGP Sirro, amewahakikishia askari na maofisa
kuwa, yupo tayari kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza na
kuwataka askari kuongeza kasi ya kukabiliana na matishio ya kiuhalifu na
wahalifu ili kuifanya jamii kuishi kwa amani na utulivu.
Aidha,
katika ziara hiyo, masuala mbalimbali yamejadiliwa huku mbinu mpya za
kukabiliana na uhalifu katika mkoa huo pamoja na wilaya zake zikiibuliwa
kwa kuzingatia kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
No comments:
Post a Comment