Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo
akizungumza na wajasiriamali wa Manispaa ya Dodoma katika hafla ya
kukabidhi hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya vikundi vya Kinamama na
Vijana.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma
Godwin Kunambi akitoa taarifa ya mikopo ya vijana na kinamama kwa Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Meya wa Manispaa ya Dodoma Profesa
Davis Mwamfupe akimkaribisha Nabu Waziri Ofisi ya Rais, Selemani Jafo
kuzungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya
vikundi vya kinamama na vijana.
Mwakilishi wa kikundi cha vijana akimpongeza Naibu Waziri kwa maelekezo aliyoyatoa.
Mmoja wa kinamama wajasiriamali akitoa shukrani kwa serikali baada ya kuwezeshwa.
Wawakilishi wa vikundi vya vijana
na kinamama wa Manispaa ya Dodoma wakipokea hundi ya Sh.Milioni 70 kwa
ajili ya shughuli za ujasiriamali.
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tamisemi Selemani Jafo amezitaka halmashauri kuwawezesha vijana na
kinamama kwa vitendo kwa kuyapa makundi hayo baadhi ya kazi zilizo
chini ya halmashauri ambazo wanao uwezo wa kuzifanya ili wajiongezee
kipato.
Jafo ameyasema hayo leo katika
hafla ya kukabidhi hundi ya Sh. milioni 70 iliyotolewa na Manispaa ya
Dodoma kwa vikundi vya ujasiliamali vya vijana na kinamama ndani ya
manispaa hiyo.
Ameeleza kwamba haipendezi kwa
halmashauri yeyote kuwanyima fursa ya kazi vikundi vya vijana na
kinamama ambapo kazi hizo zinaweza kufanywa na makundi hayo.
Jafo ametolea mfano kikundi cha
vijana cha DOYODO ambacho kina kiwanda cha kisasa cha kufyatua Matofali
lakini wanahangaika soko la kuuzia matofali wakati kuna ujenzi mkubwa
wa madarasa na vyoo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
“Kwa mfano kuna ujenzi unatarajia
kuanza kwenye shule za msingi za Nkuhungu, Mwenge, na Ihumwa ambapo kuna
zaidi ya vyumba 12 vya madarasa na vyoo matundu zaidi 18,”amesema
Naibu Waziri Jafo ameipongeza
manispaa hiyo kwa kuvitumia vikundi vya vijana katika utengenezaji wa
madawati ya shule za msingi na sekondari na amezitaka halmashauri
nyingine hapa nchini kuiga mfano huo.
No comments:
Post a Comment