Thursday 13 July 2017

Linex Sunday:Siwezi kuyapa nafasi tena mapenzi ya mtandaoni

Image result for Linex Sunday Mjeda
Msanii Linex Sunday Mjeda
Msanii wa bongo fleva mwenye hit song ya 'Got Me' Linex Sunday Mjeda amefunguka kwa kudai hawezi kuyapa nafasi tena mapenzi ya mtandaoni kwa kile anachokiona kwa upande wake kama kupoteza mashabiki wa muziki.
Linex ameeleza hayo baada ya kupata mtoto wa kiume aliyepewa jina la Jaheim jambo ambalo liliwashangaza wengi kutokana na msanii huyo kutowahi kumuonesha mwanamke ambaye amemzalia mtoto huyo kipindi alipokuwa mjamzito.
"Sikutaka kuweka 'tension' labda watu waone nina mtu mjamzito na nini sikutaka hivyo, hata hivyo nilikuwa sipendi kumuonesha mtoto wangu ila nimelazimishwa sana na watu ndiyo maana nikamuweka ili nisije kuonekana nilikuwa nina nia mbaya", amesema Linex
Pamoja na hayo, Linex aliendelea kwa kusema "Kuna vitu vya kujiuliza unajua kuna mashabiki wanaona kwamba leo umekuwa na mtu fulani kesho unatoka na fulani sidhani kama inajenga picha nzuri halafu pia mapenzi ya 'Publicity' siyo kitu poa na ndiyo maana mimi sasa hivi katika vitu ambavyo siwezi kuvifanya ni ku-date na staa yaani siwezi kudate na mtu yeyote ambaye labda ana umaarufu katika 'social network' hizo 'deal' sitaki kabisa, nataka kuishi 'normal life'", amesisitiza Linex.

Kwa upande mwingine Linex amesema ameamua kubadilisha 'style' nzima ya maisha yake kutokana na muda kumtupa mkono.

No comments:

Post a Comment