Friday, 21 July 2017

Habari Picha

1
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kushoto)  akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizoharibu  tabaka la ozoni (Refrigerant Identifier)  kwa Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi stadi (VETA) Bwana Daudi Kadinda wakati wa makabidhiano Ofisini kwa Mkurugenzi huyo.
2
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kushoto) akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kwa Afisa toka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bwana Arnold Mato, wakati wa makabidhiano Ofisini kwa Mkurugenzi huyo.
3
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akipeana mkono na Wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  na Chuo cha ufundi Stadi VETA-Chang’ombe mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya vinavyotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizoharibu  tabaka la ozoni.
4
Pichani kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kinavyoonekana kwa ndani.
5
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais  Bibi Magdalena Mtenga akijadiliana jambo na Wawakilishi toka TBS na VETA-Chang’ombe mara baada ya makabidhiano hayo.

No comments:

Post a Comment