Mkurungezi mtendaji Mkuu wa
(GEL) Abdulmalick Mollel akimuelezea Huduma za Taasisi hiyo Dr.Charles
Msonde ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa Mitihani( NECTA)
wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonyesho ya vyuo vikuu
yaliyoandaliwa na (TCU) Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa Taasisi ya Global
Education Link Bw. Liberius John akiwa anatoa maelezo kwa wateja
waliotembelea banda hilo ili kujionea huduma zinazotolewa na (GEL)
Baadhi ya wanafunzi na wananchi
waliotembelea maonyesho hayo wakipata maelezo wakati walipotembelea
banda la Global Education Link.
Wafanyakazi Mbalimbali wa Taasisi
ya Global Education Link wakiwa kwenye banda hilo kwa ajili ya kutoa
huduma kwa wananchi wanaotembelea maonyesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Maonyesho hayo
yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)
Global Education Link (GEL) ambao
ni mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imesema kuwa kwa wanafunzi wanaotaka
kufanyiwaudahili ili kujiunga na vyuo vikuu vya nje wanaweza kufika
katika banda la na kupata maelezo hukusu vyuo hivyo katika maonesho ya
TCU jijini Dar es salaam ,wanafunzi,wazazi na walezi mnakaribishwa ili
kupewa miongozo ya udahili wa vyuo vikuu nje ya nchi,katika ngazi ya
diploma mpaka shahada ya udhamili.
Akizungumza Mkurungezi wa Global
Education Link(GEL),Abdulmalik Mollel amesema katika dhima ya serikali
ya awamu ya tano ya viwanda inahitajika rasilimali watu wa kutosha ili
kukidhi mahitaji hayo
Mollel amesema wanafunzi
wanaohitaji kwenda kusoma nje ya nchi wajitokeze katika viwanja vya
Mnazi Mmoja na kukutana na timu nzima ya Global Education Link kwa
ushauri na utaratibu wa udahili wa papo kwa papo.
No comments:
Post a Comment