Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral Sunil Lanba Ofisini
kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kulia ni Mkuu wa Majeshi,
Jeneral Venance Mabeyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba (kulia
kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai
28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venace Mabeyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akijadili jambo na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral Sunil Lanba
(kulia) baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es
salaam Julai 28, 2017 . Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Nchini, Jeneral
Venance Mabeyo na kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil
Lanba (wapili Kushoto) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance
Mabeyo (kushoto) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini
Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini,
Sandeep Arya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil
Lanba (kulia kwake ) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance mabeyo
(kushoto kwake ) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu
jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini,
Sandeep Arya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WaziriMkuu Kassim Majaliwa
amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya
India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.
Ametoa kauli leo (Ijumaa,
Julai 28 , 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa
India, Bw. Admiral Sunil Lanba jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema Tanzania
na India ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu, ambapo
ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.
“Ushirikiano wa Tanzania na India
ni wa kihistoria, hivyo tutauendeleza na kuudumisha. India
tunashrikiana nao katika sekta za uchumi, afya, elimu na ulinzi.”
Waziri Mkuu ameishukuru Serikali
ya India kwa ufadhili walioutoa kwa Tanzania katika kuimarisha miradi
ya maji kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Pia Waziri Mkuu amewakaribisha
raia wa India kuja kutembelea maeneo ya utalii nchini ukiwemo mlima wa
Kilimanjaro, mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.
Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi
wa India, Bw. Lanba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano
inaoutoa kwa Serikali ya India hususan katika masuala ya ulinzi.
Amesema wamefanya kikao na Mkuu wa
Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo ambapo katika mazungumzo yao
wameweka mikakati ya kushirikiana katika kuimarisha ulinzi hususan
maeneo ya mipakani pamoja na masuala ya mafunzo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JULAI 28, 2017
No comments:
Post a Comment