Watayarishaji wa filamu kutoka
makampuni mbalimbali wakiangalia moja ya kifaa kinachotumika kuandaa
filamu katika Studio za Wanene Entertainment walipotembelea studio hizo
katika kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es Salaam.
Kushoto waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Bibi. Joyce Fissoo akijaribu kupiga ngoma zinazotumika kuandaa kazi za
muziki na filamu katika Studio ya Wanene Entertainment wakati wa ziara
iliyofanywa na watayarishaji wa kazi za filamu kuboresha ubora wa filamu
nchini Jana Jijini Dar es Salaam.
Watayarishaji wa filamu kutoka
makampuni mbalimbali wakiangalia moja ya chumba kinachotumika kuandaa
filamu katika Studio za Wanene Entertainment walipotembelea studio hizo
katika kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Watayarishaji wa filamu kutoka
makampuni mbalimbali, watendaji kutoka Bodi ya Filamu pamoja na
watayarishaji kutoka Studio ya Wanene Entertainment katika picha ya
pamoja wakati wa ziara iliyofanywa na watayarishaji hao katika Studio
za Wanene Entertainment kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar
es Salaam.
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Wazalishaji wa kazi za filamu
nchini wametakiwa kuzalisha kazi zenye ubora na viwango vinavyotakiwa
ili Tanzania iweze kupambana na mataifa mengine katika sekta ya filamu.
Rai hiyo imetolewa na Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo wakati wa ziara iliyofanywa
na Bodi ya Filamu pamoja na makampuni mbalimbali ya watayarishaji Jana
Jijini Dar es Salaam katika Studio ya Wanene Entertainment.
“Ili kuleta maendeleo chana ndani
ya Sekta ya Filamu hatuna budi kuwa mabalozi wa tasnia hii kwa
kuboresha ubora wa filamu zetu na kuweza kuliteka soko la ndani na nje
ya nchi” alisema Bibi. Fissoo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Kampuni ya Wanene Entartainment Bw. Darsh Pandit amesema kuwa kampuni
ya Wanene imekubali kushirikiana na watayarishaji wa filamu za ndani ili
kutoa filamu zenye ubora ambazo zitaleta mapinduzi kwenye tasnia ya
filamu nchini.
Kwa upande wao watayarishaji wa
ndani wa kazi za filamu wameliomba Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)
kuanzisha kitengo maalum cha kutafsiri filamu za kitanzania ili ziwe na
tafsiri inayoendana na kazi husika.
Wazalishaji wa filamu kutoka
makampuni mbalimbali hapa nchini wametembelea studio hiyo ili kuweza
kuangalia uwezekano wa kushirikiana katika kuzalisha filamu zenye ubora
kupanua wigo wa tasnia ya filamu hapa nchini.
Baadhi ya Watayarishaji
waliofanya ziara hiyo katika Studio za Wanene Entertainment ni pamoja na
kampuni za Inspiration Image, Cut2cut Entertainment, 5 Effects, Steps
na UWAFIMU.
No comments:
Post a Comment