Kamishna Jenerali wa Mgereza – CGP
John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji
wa masuala ya Kilimo cha kisasa mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake
leo Novemba 2, 2016, Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Meneja wa Kanda
ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane
Lei(kushoto) ni Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw.
Dan Ngowi.
Na; Lucas Mboje, Jeshi la Magereza – Dar es Salaam
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la
Magereza nchini, John Casmir Minja amekutana na Wawekezaji wa Kampuni ya
CAMCE kutoka nchini China pamoja na Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION
na kumuahidi kushirikiana na Shirika la Uzalishaji Mali la
Magereza(Prisons Corporation Sole) kuwekeza katika miradi
mbalimbali ya Kilimo cha kisasa, Madini na Viwanda vinavyoendeshwa na
Shirika hilo.
Akizungumza na Wawekezaji hao leo
asbuhi Ofisini kwake (Jumatano, Novemba 2, 2016) alisema kwamba Jeshi
la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji mali lina fursa nyingi za
miradi ya uwekezaji kwenye sekta nyingi kama vile Kilimo, Viwanda na
Madini ambapo aliwahahakishia ushirikiano wa kutosha kwenye uwekezaji
wao
Wawekezaji hao tayari wamefanya
mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo
wanatarajia kuiingia Makubaliano (MoU) na Jeshi la Magereza kwa ajili ya
miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo cha kisasa katika Gereza Idete
lililopo Mkoani Morogoro pamoja na Mradi wa Ngo’mbe wa nyama Gereza
Ubena, Mkoani Pwani.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya
Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei
alisema amefurahishwa na ziara waliyofanya nchini na wapo tayari
kuwekeza hapa Tanzania.
Naye, Mwakilishi wa Kampuni ya
Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi ambayo inashughulikia na masuala
ya Kilimo cha mazao ya chakula na nyama alisema watawekeza kwenye kilimo
hususan cha umwagiliaji na watajenga Kiwanda kwa ajili ya usindikaji.
Shirika la Uzalishaji mali la
Magereza(Prisons Corporation Sole) lina jumla ya Miradi 23, kati ya hiyo
miradi 15 ni ya kilimo na mifugo na 8 ni ya viwanda vidogo vidogo, pia
zipo shughuli za mradi wa Kikosi cha Ujenzi zinazosimamiwa na Shirika
hilo.
Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi
sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali pamoja na kuchangamkia
fursa zilizopo ikiwemo uwekezaji wa ubia kwenye miradi yake ili
kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa
majukumu yake
No comments:
Post a Comment