

Rais
mteule wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ni ”heshima” kubwa
kukutana na rais Barrack Obama katika mazungumzo ya mpito yaliofanyika
katika ikulu ya White House.
Bwana Obama amesema kuwa ametiwa moyo kuhusu mazungumzo yao ya maswala mbalimbali yaliochuua zaidi ya saa moja.
Bwana Trump ametilia shaka uraia wa rais Obama na kuapa kuharibu ufanisi wake wakati wa utawala wake.
Wakati wa kampeni bwana Obama alisema kuwa bwana Trump ‘hafai’ kuongoza Marekani.
Hatahivyo Obama alisema kuwa ”anamuunga” mkono baada ya kumshinda Hillary Clinton.
Alisema kuwa wamezungumza sera za
nyumbani pamoja na zile za kigeni na kwamba amefurahishwa na maoni ya
Donald Trump kwamba yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika
maswala yanayokabili Marekani.
Bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika siku zijazo
No comments:
Post a Comment