Sunday, 20 November 2016

Omog aanika ripoti yake

Kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog amewasilisha ripoti yake ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Soka Bara kwa uongozi wa klabu hiyo huku akitoa mapendekezo yake kadhaa.
Omog aliiongoza Simba na hadi ligi inamaliza mzunguko wa kwanza, ikiongoza kwa pointi 35 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 33.
Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele  kuwa wameipokea ripoti hiyo na Kamati ya Utendaji imeanza kuyafanyia kazi mapendekezo mbalimbali.
Alisema kati ya mapendekezo hayo ni kutaka wasajiliwe wachezaji wawili, golikipa na mshambuliaji ili kuboresha maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment