Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai
amekiri uwepo wa wabunge wapya kwenye bunge la 11 ambao ni asilimia 70
ya wabunge wote ni changamoto kubwa katika uendeshaji wa vikao vya
muhimili huo kwani wengi wao bado hawajui majukumu yao kutokana na
kutozifahamu kanuni.
Mhe Ndugai anabainisha changamoto hiyo mbele ya wajumbe kutoka nchi za
jumuiya ya Nordic pamoja na washirika wa maendeleo kutoka shirika la
maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) ambao ni wafadhili wa mradi wa
kuwajengea uwezo wabunge na watumishi walipomtembelea ofisini kwake
ambapo amesema wabunge wapya wanahitaji mafunzo ya kina kuhusu masuala
ya kibunge
Kwa upande wake mkuu wa msafara wa wajumbe hao ambaye ni muwakilishi wa
UNDP nchini Alvaro Rodriguez amesema pamoja na mambo mengine ujumbe huo
unaamini kupitia bunge la Tanzania itafikia malengo yake endelevu
ifikapo mwaka 2030 huku wakipongeza mpango wa Tanzania wa kutaka kuwa na
asilimia 50 kwa 50 ya wabunge wanaume na wanawake.
Aidha ujumbe huo pia ukatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo chini ya
ufadhiliwa na UNDP pamoja na wajasiriamali ikiwemo wasindikaji wa
mafuta ya alizeti kanda ya kati ambao wameomba serikali na wahisani hao
kuangalia namna ya kuongeza thamani ya bidhaa hiyo ili iweze kumudu soko
la ushindani la ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment