Chama cha mpira wa miguu cha England FA kimemshtaki kocha Jose Mourinho
kwa utovu wa nidhamu alioonesha katika mechi ya Man United dhidi ya
Burnley jumamosi ya, Oktoba 29,2016.
Imeripotiwa kuwa kipindi cha mapumziko Kocha huyo alitumia maneno mabaya
kwa mwamuzi Mark Clattenburg,na kipindi cha pili akapelekwa jukwaani
kwa mashabiki kutokana na kosa hilo.
Jose alikuwa mkali kwa mwamuzi huyo akidai kwa nini timu yake haikupewa
penati pale Matteo Darmian alipochezewa vibaya na Jon Flanagan katika
eneo la hatari.
FA imemtaka Jose kujibu shtaka hilo kabla ya siku ya ijumaa ya juma hili.
No comments:
Post a Comment