Ikulu ya Marekani imeingia katika mgogoro ambao umetikisa kampeni za urais, katika hatua za kufunga kampeni hizo.
Rais Obama amesema hamuamini mkurugenzi wa shirika la upelelezi nchini
humo, James Comey,na kuwa anajaribu kushawishi matokeo ya uchaguzi huo.
Viongozi wa juu wa Democratic wamemkosoa vikali Bwana Comey baada ya
shirika la upelelezi wiki iliyopita kusema kuwa lilikuwa likichunguza
iwepo wa barua pepe mpya zilizogunduliwa zaweza kumuhusu Bi Clinton.
Shirika hilo limeongeza kuwa wanachunguza ili kuona iwapo zimejumuisha taarifa za siri.
Mapema uchunguzi wa shirika la upelelezi la Marekani lilisema kuwa
watumishi wa barua pepe binafsi ya Bi Clinton walizifuta barua za makosa
ya kihalifu za Bi Clinton.
Akiongea mjini Ohio, Bi Clinton amesema kuwa alikuwa na uhakika kwamba
shirika hilo la upelelezi lingesema hivyohivyo kwa mara nyingine.
No comments:
Post a Comment