Na: Frank Shija, MAELEZO.
Serikali ya pongezwa kwa hatua ya kuridhia makubaliano ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, Paris 2015 UN Climate Change Conference COP21.CMP11.
Pongezi
hizo zimetolewa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mhadhiri wa Heshima wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere 2016, Mhe.
Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akitoa muhadhara katika Tamasha la
Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na Mabadiliko ya Hali ya
Hewa leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Bilal amesema kuwa kitendo cha Tanzania kuridhia makubaliano haya ya Paris kina maana kubwa sana katika suala zima la kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia nchi na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
“Niipongeze
Serikali yetu kwa kuridhia kuingia katika makubaliano ya Paris ya mwaka
2015 hii itakuwa hatua muhimu sana katika jitihada za kukabiliana na
changamoto za mabadiliko ya tabia nchi”. Alisema Dkt. Bilal.
Aidha
Dkt. Bilal aliongeza kuwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa ni
makubwa sana hivyo ni vyema tukachukua tahadhari kubwa katikakuhakikisha
tunakabiliana nayo.
Tuweke
utamaduni wa kuhifadhi na kuyatunza mazingira yetu ili vizazi vijavyo
visije kupata taabu itokanayo na uharibifu wa mazingira unaoweza
kuepukika.
Hakikisheni
mnatunza mazingira kwani kufanya uharibifu kunapoteza uhakika wa maisha
kwa viumbe hai, pamoja na kupoteza vyanzo vya mapato,hivyo ni vyema
tukajiepusha na matumizi ya baruti, uvuvi haramu, ukataji miti na
mikoko.
Kwa
upande wake Balozi wa Norway nchini Balozi Hanne – Marie Kaarstad,
amesema kuwa Tamasha la Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira
na Mabadiliko ya Tabia nchi limekuja wakati muafaka ambapo dunia
imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Amesema
kuwa Tanzania inaeneo kubwa la mwambao ambalo lina ulinzi wa asili
hivyo ni vyema kuvilinda kwa kufanya usafi ilikuendeleza uhai wa viumbe
hai vilivyopo majini na nchi kavu.
Naye
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na
Mabadiliko ya Tabia nchi Profesa. Pius S. Yanda alisema kuwa Tamasha
hilo limewakutanisha wadau kutoka nchi za Afrika Mashariki kwa lengo la
kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia
nchi.
Profesa
Yanda aliongeza kuwa wataendelea kushirikiana baina ya nchi za Afrika
kama na huu ndiyo mwanzo mzuri tulioanza nao, pia alitumia fursa hiyo
kuipongeza Serikali ya Norway kwa shirikiano wao katika Nyanja ya
mazingira ambapo alisema Norway inafadhili takribani PhD 11 katika eneo
la mazingira.
No comments:
Post a Comment