“Juu ya yote hayo uliyofanya lengo ni kutaka watoto wa kike na wenyewe wawe na kiwanja cha mpira hongera sana kidoti, hili jambo huwa sio rahisi sana, tuna watu wangapi wanaweza kutengeneza viwanja kama hivi hata kumi, lakini wewe kwa kile kidogo ulichokipata ukasema hapana mimi ujuzi wangu na experience na yale niliyopata ngoja nisaidie,”, alisema Bi. Mjema.
Awali Mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo alisema, “Mimi naamini michezo ni kitu hamasishi kwa wanafunzi kufanya vyema pia katika masomo yao na kufaulu ni wazi kuwa moja ya changamoto kubwa nchini. Ukosefu wa viwanja bora ambavyo hukwamisha wachezaji chipukizi kuonyesha vipaji vyao ipasavyo,” alisema Jokate.
Alisema ataendelea kujenga viwanja katika shule mbalimbali kwa faida ya wanafunzi. Jokate ameshiriki ujenzi wa uwanja huo akishirikiana na taasisi ya Modern Foundation.
No comments:
Post a Comment