Thursday, 25 August 2016

Viongozi 98 wa vyama vya ushirika kusimamishwa

William Ole Nasha

Naibu Waziri Ole Nasha ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na EATV ilipotaka kujua utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kutaka wizara hiyo ichukue hatua kwa watendaji wabovu wa vyama hivyo na kusababisha hasara kubwa ya fedha kwa taifa.

Amesema sambamba na hilo serikali imeweka sheria mpya kwa vyama vya ushirika ya kudhibiti ubadhirifu wa fedha na kudhibiti wizi kwa kuweka mifumo maalum ya kuangalia mapato ya vyama vyote vya ushirika na kubuni njia bora ya kuendesha vyama hivyo ili visiendelee kuliingiza taifa hasara ya fedha ambazo kama zikikusanywa vizuri zitapelekwa kuboresha maisha ya watanzania.

Amesema sheria hiyo imeanza kutekelezwa na kuahidi kutowavumilia wale wote wanaoiba fedha za umma
.

No comments:

Post a Comment