Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza
na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabati kabla ya kuchangia
damu katika hospitali hiyo LEO.
Balozi wa Palestina nchini
Tanzania, Hazem Shabati akichangia damu LEO katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH). Kulia ni mtaalamu kwa kutoa damu katika hospitali hiyo,
Sabastian Magulu.
Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabati
amewataka Watanzania kuwa na tabia ya kuchangia damu ili kuokoa maisha
ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Balozi Shabati amefika LEO katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) kwa ajili kuchangia damu na kuwahamasisha watu
wajitokeze kwa wingi ili kuchangia damu.
Amesema kila mtu ana wajibu wa kuchangia damu kwa kuwa ni muhimu kwa maisha ya wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.
Pia, Balozi Shabati amesema lengo la kuchangia damu ni
kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na nchi yake ambao ni wa muda mrefu
na wa kihistoria.
Katika hatua nyingine, Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo,
Neema Mwangomo amesema kwa wastani hospitali hiyo inakusanya chupa 40
hadi 50 kwa siku, lakini mahitaji kwa siku ni chupa 80 hadi 100.
Amesema makundi makubwa yanayohitaji damu kina mama
wajawazito, watoto wenye saratani, majeruhi wa ajali na wagonjwa
wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji.
Mwangomo amesema mwanaume mwenye umri wa miaka 18 hadi 65 ndiye anapaswa kuchangia damu wakati mwanamke ni miaka 18 hadi 62.
Amesema kigezo cha pili ni mtu anayechangia damu anapaswa
kuwa na uzito wa kilo 50 na kuendelea na kwamba mtu anapaswa kuwa na
wingi wa damu kuanzia asilimia 85.
Mwanamke anaweza kuchangia damu mara tatu kila baada ya miezi minne wakati mwaume mara nne kila baada ya miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment