Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha
Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto), akizungumza na
waandishi wa habari jijini kuhusu tuzo za Mwajiri Bora 2016
zinazotarajiwa kutolewa mwezi Disemba mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika
katika ofisi za ATE,jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko,
Mawasiliano na Mradi, Joyce Nangai.
Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na
Mradi, wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Joyce Nangai (kushoto)
akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka.
Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakirekodi wakati Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk Aggrey Mlimuka
akizungumza nao kuhusu tuzo za mwaka huu za Waajiri Bora zinazotarajiwa
kutolewa baadae mwaka huu.
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
leo kimezindua Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2016 kutambua Waajiri wenye
misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu ili
kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji
kibiashara.
Akizungumza kwenye Mkutano na
Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka
alisema kwamba lengo kuu la Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka ni kutambua
wanachama wenye sera nzuri za usimamizi wa rasilimali watu.
Alisema kuwa kwa miaka kadhaa tuzo
hiyo imesaidia kuhamasisha wanachama kujikita katika kushughulikia
masuala ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama msingi muhimu
katika kumwezesha mwajiri kuwa na wafanyakazi wenye kukikidhi ushindani,
wanaojituma na wenye furaha.
Aliongeza kuwa tuzo hiyo ilifuata
mbinu za kisayansi na kitaalamu ili kuangalia umuhimu wa Rasilimali
Watu katika makampuni ya kibiashara kuanzia makampuni makubwa kwa
madogo na yale ya kati ili kuinua ujuzi na kuwa na wafanyakazi wenye
kufanaya kazi kwa kujituma kama njia ya kutoa motisha kwa wafanyakazi
ambao ndio msingi wa rasilimali watu.
Aliongeza kuwa EYA lilikuwa tukio
muhimu linalofanywa na ATE kila mwisho wa mwaka tangu mwaka 2005.
Alisema kuwa tuzo hiyo imekuwa maarufu hapa nchini katika muktadha wa
biashara hasa kwa kuhamamasisha makampuni makubwa na madogo na ya ukubwa
wa kati kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya kufanya biashara
nchini.
Aliongeza kuwa tukio hilo la
kutafuta mshindi limegawanyika katika makundi makuu mawili ambapo
litaanza na kufanya utafiti kwa kutumia Mshauri Mwelekezi na hatua ya
pili itakuwa ni hafla ya kutoa tuzo yenyewe kwa washindi ambalo
litafanyika mwezi Desemba 2016.
“Tukio hili limegawanyika katika
makundi mawili, ambapo hatua ya kwanza ni kufanya utafiti na hatua ya
pili ni hafla ya kutoa tuzo kwa washindi,” alisema.
Aliwaomba pia Wanachama kushiriki
kwa wingi ili kuweza kushindana na waajiri wengine kupitia shughuli
wanazozifanya. Aliongeza kuwa kwa mwaka huu waajiri wataweza kujifunza
kupitia kile kinachofanywa na makampuni mengine ili kuhakikisha wanakuwa
na wafanyakazi wenye wanaojituma na wenye furaha katika kufanya kazi.
Dkt. Mlimuka alisema kuwa Tuzo ya
Mwajiri Bora wa Mwaka 2016, ilikuwa ya 9 tangu kuanza kwake na kuaongeza
kuwa tuzo hiyo kwa mwaka huu itakuwa ya tofauti kulinganisha na zile
zilizotangulia kwa kuwa itahusisha tuzo nyingine mbili mpya mojawapo
ikipima Ushiriki wa Wafanyakazi ili kujua ni kwa kiasi gani wafanyakazi
wanajihusisha na kazi wanazofanya, wanajitoa kwa ajili ya waajiri wao,
na kama wana bidii katika utendaji kazi wao.
Alisema kuwa tuzo nyingine mpya
ilikuwa ikiangalia umuhimu wa Usimamizi wa Vipaji na Kuviendeleza na
lengo lake ni kuyawezesha makampuni kuvutia, kutunza, kutoa motisha na
kuendeleza majhitaji ya wafanya kazi kwa sasa na siku za usoni
“Tumeanzisha tuzo mbili mpya kwa
mwaka huu ili kuwawezesha waajiri kuboresha mazingira ya biashara
kuhakikisha wafanyakazi wao wanashiriki kikamilifu katka utendaji kazi
na hivyo kumwezesha mwajiri kupata na kuvutia waafanyakazi wenye ujuzi
stahiki kwa manufaa ya sasa na siku za usoni,” alisema Dkt. Mlimuka.
Alisema kuwa tuzo hiyo imekuwa
ikijikita katika kuangalia maeneo muhimu ya kusimamia Rasilimali Watu
kama vile Uongozi na Utawala, Usimamizi wa rasilimali watu, Kusaidia na
Kuwajibika kwa Jamii, Ubora na Uzalishaji, Kushirikisha Watu Wenye
Ulemavu na Kujali Wafanyakazi.
Akizungumzia kuhusu namana ya
kushiriki katika tuzo hiyo, Dkt. Mlimuka alishauri wanachama kushiriki
kwa kujaza dodoso kupitia njia mojawapo kati ya njia tatu ambazo ni kwa
njia ya umeme (Electronically), kwa njia ya mtandao (Online), au kwa
kuwasilisha dodoso zilizojazwa kwa mkono.
Alikumbusha kuwa wanachama wwanaopenda kushiriki dodoso kupitia anuani ya: www.eya2016.co.tz
ili kushiriki katka tuzo hii muhimu sana. Alisema kuwa mwisho wa
kujaza dodoso za ushiriki itatakuwa Ijumaa tarehe 30 Septemba 2016.
Mwaka jana Tuzo ya Mwajiri Bora wa
Mwaka ilifanyika kwa mafanikio makubwa ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe.
Kassim M. Majaliwa (MB) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ushiriki uliongezeka kwa 100% kulinganisha na mwaka uliopita na kwa
mwaka huu tunategemea idadi ya washiriki itaongezeka mara dufu.
Makampuni mengi yalishiriki katika tuzo hiyo na baadhi ya washiriki
walishinda tuzo hiyo na kati ya washindi hao alikuwa Tanzania Brewies
Ltd (TBL), CCBRT, Kilombero Sugar Company, Social Security Regulatory
Authority, Yakubu & Associates Chambers, Total Tanzania Ltd, TIGO
Tanzania, CRDB Bank Plc na Geita Gold Mine. Kwa taarifa zaidi kuhusu EYA
iliyopita tembelea www.eya.oc.tz. Mwaka huu tunategemea kuwa wanachama wengi zaidi watashiriki na wanasubiri tuzo hii kwa shauku kubwa.
No comments:
Post a Comment