Mohamed Dewji anapendekeza kuwa yeye atatoa tshs 20bn na kuziweka kwenye Endowment Fund kisha riba kutumika kuendesha Club. Tutakuwa na club matata sana nchini. Vyuo vikuu vikubwa duniani Kama Harvard vinaendeshwa kwa Mfumo huu anaopendekeza MO. Tukiwa na usimamizi mzuri wa Fedha tutakuwa timu bora kabisa na tutaweza hata kuwa na academy ya Simba Kama ilivyo kwa club kubwa duniani.
Hata hivyo, nashauri kwenye muundo wa umiliki, mtu mmoja asiwe na Hisa zaidi ya 40%. Ushauri wangu ni mgawanyo ufuatao;
– Mwekezaji ( MO ) 40% ( mkataba wake wa uwekezaji uonyeshe kuwa kwa kupewa Hisa hizi atafungua endowment fund ya thamani ya tshs 20bn na atakuwa na uhuru wa kuteua trustees wa Fund hiyo. Mwekezaji atakuwa na uhuru wa kuifunga fund iwapo asiporidhishwa na matumizi Fedha zinazotokana na Endowment Fund ).
– 20% ya Hisa ziorodheshwe kwenye Soko la Hisa la Dar Es Salaam kwa ajili ya 1) kuvutia wawekezaji wengine 2) kukuza mtaji wa Kampuni 3) kuwezesha uwazi kwenye uendeshaji wa kampuni kwani Wanachama wote watakuwa wanajua kila kinachoendelea kwenye kampuni na club kwa sababu soko la Hisa Lina ‘ disclosure rules ‘.
Nashauri wana Simba tusicheleweshe haya MABADILIKO. Tufanye sasa hivi ili msimu huu unaoanza tuwe na timu imara yenye uhakika wa kushiriki Premier League. Mpango wa MO wa Endowment Fund ni Mpango bora na tusipoteze nafasi hii.
No comments:
Post a Comment