Friday, 26 August 2016

Mahakama nchini Zimbabwe imeamuru wapinzani waendelee na maandamano leo

Polisi wa kutuliza ghasia tayari wametumia gesi za kutoa machozi dhidi ya watu waliokuwa wakijiandaa kwa maandamano.
Mahakama ya kuu nchini Zimbabwe imeamua kuwa maandamano ya ya makundi ya upinzani yanaweza kuendelea hii leo, kati ya saa sita mchana na saa adhuhuri .
Jana polisi walionya kuwa maandamano yoyote ambayo hayajaidhinishwa hayatakubalika.
Polisi kikosi cha kutuliza ghasia tayari wametumia gesi za kutoa machozi dhidi ya makundi madogo ya watu waliokuwa wakijiandaa kwa maandamano.

Maandamano ya leo yameandaliwa na makundi kadhaa ya upinzani yaliyo katika muungano unaojiita NERA - unaodai mageuzi ya sheria za uchaguzi - wanaosema wanataka kufana maandamano ya amani kutoa wito wa kufanya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi .

Zimbabwe imekua ikishuhudia maandamano makundi makubwa ya umma katika kipindi cha miezi kadhaa, zaidi yakielezea kutoridhishwa na hali ya uchumi wa nchi yao uliodidimia.

Chama kikuu cha upinzani cha MDC na upinzani mpya unaoongozwa na makamu rais wa zamani Joice Mujuru wa chama cha Zimbabwe People First,ni miongoni mwa makundi yanayoshiriki maandamano ya leo.

No comments:

Post a Comment